KAMANDA DIWANI
Mkazi mmoja wa Kiwira kata ya Kiwira
wilaya Rungwe mkoani Mbeya Bw. Joseph Mwaenga (32) ambae ni mwendesha
piki piki anusurika kujilipua na kulipua kituo cha polisi akipinga
vitendo vya uonevu vinavyofanywa na askari hao.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya
Diwani Athuman amewaeleza wanahabari leo kuwa tukio hilo limetokea
jana majira ya 5 usiku katika eneo la kituo hicho .
Alisema kuwa kijana huyo ambae ni
mwendesha boda boda alifikishwa kituoni hapo baada ya kufanya vurugu
katika kijiwe cha maegesho ya pikipiki na baada ya hapo alipokonywa
pikipiki yake (Boda Boda ) na wananchi na kuifikisha polisi .
Hata hivyo baada ya kufikishwa
kituoni hapo akiwa nje ya kituo alijimwagia petrol na kumwagia kituo
cha polisi kisha kutoa kiberiti na kutaka kujilipua yeye na kituo hicho
kabla ya kuthibitiwa na askari wa zamu
Kamanda Athuman alisema kuwa
mtuhumiwa huyo baada ya kufanya vurugu kijiweni wananchi
walimpokonya boda boda yake na kuipeleka kituo cha polisi na ndipo
kijana huyo alipoamua kuifuata boda boda yake kituo cha polisi huku
akiwa na dumu la mafuta ya Petrol na kiberiti na baada ya kufika nje ya
kituo hicho alijimwagia mafuta mwili mzima na kumwagia kituo cha
polisi na kisha kutaka kujitoa muhanga kwa kujilipua .
Alisema kuwa hakuna madhara
yaliyojitokeza kwa binadamu wala mali juu ya tukio hilo na mtuhumiwa
amekamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
|