OPARESHENI YA KUONDOA TENA MACHINGA UBUNGO YAFANYIKA

Wanamgambo wa Manispaa ya Kinondoni wakiendesha operesheni ya kuwakamata wafanyabiashara ndogondogo eneo la Ubungo kwenye kituo cha daladala ikiwa ni sikumoja tu tangu blog ya raha za pwani kuripoti kurejea kwa wafanyabiashara  hao kwenye eneo hilo. Leo tangu majira ya asubuhi wafanyabiashara waliliona chungu eneo hilo na kulazimika kulikimbia na wachache waliojaribu kufanyabiashara waliangukia mikononi mwa wanamgambo hao.
Eneo la Stendi ya daladala la Ubungo likiwa na utulivu bila ya wafanyabiashara hao (Wamachinga) kutokana na ulinzi uliokuwa umeimarishwa.
Utulivu na amani inakuwepo zaidi kama hakuna wafanyabiashara wadogowadogo vituo vilikuwa vyeupe kabisa.PICHA NA SAIDI POWA


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo