Na Fadhili Athumani, Moshi
WAKAZI wa Mtaa wa Dobi, Kata
ya Njoro, Wilaya ya Moshi mjini, Mkoani Kilimanjaro, walijikuta wakianza
Mwaka
kwa majonzi baada ya kijana Abdalla Mussa (22), kukutwa akiwa amekufa,
Nyumbani
katika tukio linalodhaniwa kuwa ni ya kujinyonga.
Tukio hilo la kusikitisha
lilitokea jana majira ya saa saba mchana ambapo Father Kidevu
Blog iliweza kufika katika eneo la
tukio na kukuta maiti ya Marehemu ikiwa bado imening’inizwa kwa kipande
cha
kitenge kwenye Nyumba Bovu lililo karibu na Nyumba ya Mzazi wa Marehemu.
Marehemu kwa mujibu wa Mama
Mzazi, Hawa Athumani, alikuwa anasumbulia na Malaria ambapo wiki mbili
kabla ya
tukio hilo, Marehemu alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Kilimanjaro,
Mawenzi.
“Mwanangu alikuwa anaumwa
Malaria na Baada ya kumpeleka pale Mawenzi madaktari walisema kuwa
Malaria
imepanda kichwani, alitibiwa na ijumaa iliyopita tuliruhusiwa kurudi
Nyumbani
lakini jana (juzi) alianza kulalamika kuwa kichwa kinauma,” alisema
Hawa.
Alisema kuwa siku ya tukio,
Marehemu aliamka akiwa mzima kabisa na hadi tukio la kujinyonga
linatokea
alikuwa mzima kabisa na wala hakuonesha dalili zozote za kutia wasiwasi
na
kuongeza kuwa baadae muda wa saa Saba mchana, akiwa ameenda sokoni
kufanya
maandalizi ya sikuukuu, mwanae wa kiume, alimpigia simu na kumjulisha
kuhusu
tukio hilo.
Kwa upande mdogo wa Marehemu
ambaye alizungumza na Gazeti kwa masharti ya jina lake kutotajwa
Gazetini
alisema kuwa Kaka yake muda mfupi kabla ya kufariki dunia, alikuwa
anafanya
fujo kwa majirani na kutamka wazi kuwa lazima, siku patokee msiba lakini
kutokana na kufahamu hali yake maneno yake hawakuyachukulia kwa uzito
mkubwa.
“Kaka alikuwa tayari kashajua
kufa kwake, alianza kufanya fujo na kupiga watu ovyo na kusema kuwa siku
ya leo
lazima mtu afe, sasa sisi kutokana na kufahamu hali yake wala
hatukuchukulia
maneno yake siriazi tukaona labda ni maneno tu.
“ Baadaye kama mwendo wa saa
sita na nusu mchana nilishangaa kuona utulivu usio wa kawaida na
nilipoingia
chumbani kwake sikumkuta, tukaanza kumtafuta, kidogo mtoto wa nyumba ya
jirani
akaja na kuniambia ameona kitu kimengini akwenye ile nyumba bovu pale,
tulienda
kuangalia ni nini na kukuta kaka amekufa,” alisema Mdogo huyo wa
Marehemu.
Akizungumza tukio hilo
Mwenyekiti wa Mtaa huo, Lucy Peter Asenga, alisema kuwa, mara baada ya
kupata
taarifa za msiba huo, aliwasiliana na Jeshi la Polisi kuomba msaada
lakini cha
kushangaza pamoja na kutoa Taarifa mapema, msaada walikuja kuupata masaa
mawili
baada ya kutoa Taarifa.
Akionesha masikitiko yake
katika utendaji na ushirikiano wa Jeshi hilo mwemnyekiti huyo alisema
kama
utaratibu wa kutoa msaada wa Jeshi la polisi hautabadilishwa itafikia
muda
ambapo wananchi watatafuta msaada kwengine au kujichukulia hatua wenyewe
jambo
ambalo ni hatari kwa usalama wa Nchi.
Akithibitisha kutokea kwa
tukio Hilo, Kamanda wa Polisi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,
Robert
Boaz alisema mwili wa Marehemu tayari umaeshahidhiwa katika chumba cha
Kuhifadhia Maiti ya Mawenzi na kuongeza kuwa Uchunguzi wa chanzo cha
kifo hicho
kinaendelea.
Kamanda Boaz alitumia Nafasi
kuwataka wananchi kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha huku
akito
pole kwa Famila ya Marehemu kwa Msiba huo uliowakuta.
Source:Father kidevu