
Naibu Waziri wa
TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akipima kwa tape maalum urefu wa moja ya
barabara zilizojengwa na Manispaa ya Sumbawanga katika Mji huo
kuhakikisha kama barabara hiyo imejengwa kwa vipimo vilivyoanishwa
kwenye mpango wa ujenzi huo (BOQ). Naibu Waziri huyo alitumia fursa hiyo
kuziasa halmashauri zote nchini kusimamia vyema fedha za Serikali
katika miradi kuhakikisha inafanana na thamani ya fedha zilizotumika,
alilazimika kusema hayo baada ya kubaini mapungufu mbalimbali katika
mradi huo wa barabara na miradi mingine aliyofanikiwa kuitembelea Mkoani
Rukwa.

Naibu Waziri wa
TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akikagua barabara za lami zilizo chini ya
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga zilizojengwa hivi karibuni. Katika
ukaguzi huo alibaini mapungufu mbalimbali katika ujenzi huo na kuagiza
Halmashauri hiyo kuhakikisha mapungufu hayo yanaondolewa. Aliitaka pia
halmshauri hiyo kusimamia vyema kazi za Serikali kuepusha minong'ono
inayotoka kwa wananchi juu ya utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji
Serikalini.

Mhe. Agrey
Mwanri akiweka jiwe la msingi kiwanda cha unga cha Malangali
kinachomilikiwa na muwekezaji wa ndani mapema hivi leo. Kwa sasa Mkoa wa
Rukwa una viwanda vitatu vya unga vinavyomiliwa na wawekezaji wa ndani.

Naibu wa Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. Agrey Mwanri akikagua kiwanda cha unga cha Malangali Mjini
Sumbawanga leo alipotembelea kiwandani hapo kwa ajili ya kuweka jiwe la
msingi.

Mhe. Mwanri
akizungumza na wakazi wa Mji wa Sumbawanga katika Stendi kuu ya mabasi
ya Mjini hapo ambapo alipokea kero mbalimbali ikiwepo ubovu wa
miundombinu ya umeme na barabara katika stendi hiyo. Aliuagiza uongozi
wa Manispaa ya Sumbawanga kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi hao
kuskiliza kero zao zote pamoja na kuzitaftia ufumbuzi na kumpelekea
taarifa ya utekelezaji.

Katika hali
isiyotegemewa msafara wa Mhe. Mwanri ulipowasili katika kijiji cha
Mlanda katika Manispaa ya Sumbawanga kwa ajili ya Mkutano wa hadhara
ulikuta msiba ambapo walishiriki na kutoa ubani ambapo Mhe. Mwanri
alitoa laki moja na alfu mbili na aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini
CCM ambaye pia ni Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa ya CCM (NEC) kupitia Mkoa wa Rukwa Aeshi Hillal alikabidhi shilingi alfu hamsini.Picha na Hamza Temba -Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa