NAIBU WAZIRI AAGIZA WAKURUGENZI KUSIMAMIA TIBA BURE KWA WAJAWAZITO NA WATOTO


Na Willy Sumia, Mpanda

Serikali imewaagiza wakurugenzi watendaji wa halmashauri nchini
kuhakikisha kuwa hakuna kuwatoza wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika vituo vya kutolea huduma za afya kwenye maeneo yao

Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, mhe Aggery Mwanri katika mkutano na wananchi wa Mkoa wa Katavi uliofanyika katika viwanja vya kijiji cha Inyonga wilaya ya Mlele
januari 17, 2013

Naibu waziri huyo alisema kila kona ya nchi hii wananchi wanalalamika
kuwa wajawazito na watoto wanatozwa pesa pindi wanapofika hospitalini
kupata huduma licha ya kuwa vituo hivyo ni vya serikali na huku
serikali ikiwa imeshaeleza kuwa hakuna malipo yoyote katika vituo vya
huduma za afya vya serikali na hivyo kujengeka dhana ya kuwa serikali
inasema uongo kwa wananchi kuhusu huduma bure kwa wajawazito na watoto chini ya miaka mitano

Mwanri amewaagiza wakurugenzi watendaji wa Halmashauri, Manispaa, Miji na Majiji kusimamia kwa karibu zahanati, vituo vya afya, hospitali za
wilaya, mikoa na  za rufaa ili kuondoa kabisa kero ya wajawazito na
watoto kutozwa malipo mbali mbali kama dawa, vipimo, gloves na wakati
mwingine hata rushwa licha ya kuwa serikali imekuwa ikipeleka ruzuku
kufidia gharama hizo.

Akifafanua kisingizo cha kuishiwa dawa na vifaa Naibu Waziri Mwanri
alisema serikali kwa kuliona hilo imebadili utaratibu wa utendaji kazi
wa Bohari ya Dawa nchini MSD na kuweka ofisi za bohari hiyo katika
kanda ambapo kwa sasa kanda ya Mbeya inahudumia mikoa ya Rukwa Mbeya, Katavi, Njombe na Iringa na hivyo hakuna kisingizio cha dawa kuchelewa au kukosekana

Aliwataka waganga wakuu wa wilaya kuhamasisha wananchi kujiunga na
mfuko wa bima ya afya ya jamii CHF ili kutunisha mifuko yao na
kuongeza uwezo wa kununua dawa nyingi iwezekanavyo kulingana na
mahitaji ya eneo husika kwa wakati na kuwa na akiba ya kutosha badala
ya kusubiri dawa na vifaa ziishe kabisa ndipo waanze kuwelekeza
wajawazito, watoto na wananchi maduka ya kununua dawa

Alisema hivi sasa serikali kila kituo cha huduma kianze kuwa na
utaratibu wa kuagiza dawa kabla hazijabaki nusu ya zilizopo ili
kuepuka matatizo ya kuharibika gari njiani pamoja na kuwa na uwezo wa
kumudu mahitaji ya dharula pindi inapotokea hasa katika masuala ya
ajali na magonjwa ya milipuko inapotokea katika maeneo yao

“Ikitokea ajali katika kijiji huwa tunaanza na zahanati iliyopo
kijijini hapo wakati tunasubiri huduma za hospitali ya wilaya, mkoa na
rufaa, sasa kama mganga unakaa zahanati unasema hizi dawa zinatosha
tutakuangalia umakini wako ukoje’ alisema mhe. Mwanri

Mhe Mwanri yuko kwenye ziara ya siku saba mkoani Katavi kuanzia
Januari 15 hadi 22 mwaka huu kukagua, kutembelea, kuweka mawe ya
msingi katika miradi pamoja na kuhamasisha shughuli za maendeleo
mkoani huo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo