MIMBA SHULENI HAZIKUBALIKI - MWANRI

Na Willy Sumia, Katavi
Naibu  Waziri wa nchi  Ofisi ya waziri mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)  Mhe Aggrey Mwanri amewaagiza viongozi na Watendaji wa serikali kuhakikisha wanakomesha suala la mimba mashuleni.
Waziri Mwanri ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara katika vijiji vya  Kilida Kata ya Mamba na Inyonga wilayani Mlele Mkoani Katavi katika ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli za maendeleo katika mkoa wa ikiwa ni pamoja na kuangalia Halmashauri zinavyosimamia
fedha za serikali zinazoletwa  kwa ajili ya shughuli za miradi mbali mbali ya maendeleo.
Amesema  katika taarifa ya mkoa imeelezwa kuwa asilimia ya wanafunzi wanaopata mimba imepungua kutoka asilimia sitini na tisa hadi sitini na saba hali inayoashiria kuwa tatizo linaendelea kwa kasi sana na kuwa endapo hatua za makusudi hazitachukuliwa suala la elimu kwa watoto wa kike itaendelea kudumazwa.
Amesema kila mkoa na wilaya nchini zipo taarifa za tatizo la mimba kwa wanafunzi hivyo ipo haja ya watu kuwajibika katika kuhakikishani tatizo hili linaondoka kabisa na ni wajibu wa viongozi kuhakikisha suala la mimba linakomeshwa kabisa mashuleni na haitoshi kila mara viongozi kuripoti tu suala la mimba mashuleni bila kuchukua hatua kuchukuliwa kwa wale wahusika wanaofanya vitendo hivyo vya kuwapa
mimba watoto wa kike.
“Haitakiwi kuripoti tu, pia inatakiwa kueleza ni hatua gani
zimechukuliwa  kuhakikisha hao wanofanya vitendo hivyo wamechukuliwa hatua zipi za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo, ukisikia mimba,kamata binti mwenye mimba, kamata wazazi wake weka msukosuko watakueleza mwenye mimba” Alisema Mhe. Mwanri.
Aidha katika taarifa ya mkoa wa Katavi kwa Mhe. Mwanri imeelezwa kuwa mimba kwa mkoa wa katavi zimepungua kutoa wasichana waliopata ujauzito mwaka 2011 walikua 63  na  mwaka 2012  mimba zilikuwa  61   sawa na upungufu wa asilimia tano taarifa ambayo haikueleza namna wanavyolishughulikia tatizo la mimba na kueleza wangapi walichukuliwa hatua za kisheria kulingana na makosa hayo.
Akiwasilisha taarifa hiyo Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo, Lauteri Kanoni amesema kuwa juhudi za kuwabana wanaotenda vitendo vya kuwapa ujauzito wanafunzi zinakwama kutokana na changamoto ya baadhi ya wazazi wa mwanafunzi mwenye ujauzito kushiriki katika mikakati ya kuficha ushahidi wakati wa kumtafuta mhalifu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo