MWANAFUNZI wa kidato cha sita
katika shule ya sekondari ya wavulana ya Songea mkoani Ruvuma amekutwa
amekufa
baada ya kujinyonga kwenye mti uliopo kandokando ya njia kwenye eneo la
milima
ya matogoro ya hifadhi ya msitu ya taifa nje kidogo ya manispaa ya
Songea.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa
wa Ruvuma mrakibu mwandamizi wa polisi George Chiposi alisema kuwa tukio hilo lilitokea januari 21 mwaka
huu majira ya 12.30 asubuhi huko katika eneo la milima ya matogoro
Kaimu kamanda Chiposi alimtaja
mwanafunzi huyo aliyekutwa amekufa baada ya kujinyonga kuwa ni Ahabu
Richard Ng’ondya
(21) wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wavulana ya Songea
ambapo
alidai kuwa siku hiyo ya tukio watoto wawili ambao walikuwa wakipita
njiani
majira ya saa za asubuhi ghafla waliona kama kuna mtu ananing’inia
kwenye mti
mrefu ambao upo kandokando ya njia hiyo.
Watoto hao baada ya kuona hali hiyo
walikimbia na kukutana na mtu aliyejulikana kwa jina la Osward Kahongo
walimwonyesha tukio hilo ambaye nae pia aliwasiliana na polisi ambao
walifika
kwenye eneo la tukio wakiwa wameongozana na daktari.
Alisema baada ya polisi kufanya
uchunguzi ulibaini kuwa alikuwa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya
wavulana
ya Songea ambaye anadaiwa aliondoka kwenye eneo la shule katika
mazingira ya
kutoroka siku chache kabla ya kutokea tukio hilo.
Alibainisha zaidi kuwa upelelezi
wa awali wa polisi umebaini kuwa chanzo cha kujinyonga kwa mwanafunzi
huyo ni
kwamba alikuwa amefukuzwa shule na uongozi wa shule baada ya kutofanya
mitihani
ya majaribio hivyo uongozi uongozi wa shule ulimtaka arudi nyumbani kwao
Matamba
Uwanji wilaya ya Makete mkoani Njombe ili akamlete mzazi wake.
Alieleza zaidi kuwa baada ya
kuambiwa hivyo mwanafunzi huyo alitoeka kwenye eneo la shule na kwenda
kusikojulikana hadi hapo alipokutwa akiwa amekufa kwa kujinyonga, hata
hivyo
alieleza kuwa mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Matamba Uwanji
nyumbani
kwa wazazi wake kwa ajili ya mazishi.
