MTUHUMIWA
anayedaiwa kumuibia rais mstaafu Ally Hassan
Mwinyi sh.milioni 37, Abdallah Nassor Mzombe (40) zikiwa ni kodi ya
pango katika
nyumba mbili zinazomilikiwa na rais huyo, ameiambia mahakama ya Hakimu
Mkazi
Kisutu Dar es Salaam, kuwa anajua siri nyingi za Mwinyi ambazo kamwe
hawezi
kuzisema mahakamani hapo.
Mbele
ya Hakimu Mkazi, Jenevitus Dudu, katika utetezi
wake, mbali ya kukataa kutenda kosa hilo, Mzombe alidai amefanya kazi
nyingi na
kushirikishwa na mzee Mwinyi mambo mengi ya wazi na ya siri ambayo hata
watoto
wake wa kuzaa hawayajui na kwamba anashangazwa kuona sasa anashtakiwa
kwa makosa
ya kumuibia fedha hizo.
