Jeshi
la polisi Kanda
Maalum Dar es Salaam inawashikilia askari polisi watano kwa tuhuma za
upotevu wa
fedha kiasi cha shilingi milioni 150 mara baada ya tukio la uporaji
lililofanyika eneo la Kariakoo mnamo tarehe 14/12/2012.
Akizungumza
na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya
Polisi Dar
es Salaam Suleiman Kova (pichani) amesema baada ya tukio hilo
zilipatikana
taarifa kuwa fedha hizo zilipotea baada ya mtuhumiwa Augustino Kayula na
Frank
John Mwangiba kukamatwa akiwa na bastola aina ya Browing lakini hakuwa
na fedha
zilizoporwa, na ambaye anasemekana ndiye aliyepora fedha hizo akiwa na
wenzake.
Kamanda
Kova amesema pamoja
na kukamatwa kwa askari hao pia wamekamatwa majambazi wawili waliohusika
na
tukio hilo ambao ni ambao ni Deogratias Kimaro mkazi wa Kilakala na
Kulwa
Mwakabala Mkazi wa Kijiwesamli wilaya ya Ilala.
Watuhumiwa
hao wote
wanashikiliwa na upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na gwaride la
utambulisho.