Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza wakati akitoa maoni yake.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana
na Mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya, Jaji Joseph
Sinde Warioba, wakati tume hiyo ilipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar
es Salaam, leo kwa ajili ya kuchukua maoni yake binafsi ikiwa ni sehemu
ya kuchangia maoni ya katiba mpya.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza
wakati akitoa maoni yake kwa Viongozi wa Tume ya katiba mpya, iliyofika
Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo ikiwa ni sehemu ya jukumu
la tume hiyo la kukamilisha zoezi la ukusanyaji wa maoni ya Katiba mpya.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa tume ya Kukusanya maoni ya
Katiba Mpya, baada ya mazungumzo yao ya kupokea maoni yaliyofanyika leo
Januari 23, 2013, Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin
Sufiani-OMR
*******************************************
MAKAMU wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal amekutana na
ujumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya iliyokuwa chini ya
Mwenyekiti wake Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba pamoja
na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Agostino Ramadhan.
Makamu wa Rais amepata fursa ya kukutana na Tume hiyo Ikulu Jijini Dar
es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Warioba kabla ya
kumruhusu Mheshimiwa Makamu Wa Rais kutoa maoni yake, alimuelezea namna
tume hiyo inavyofanya kazi na namna zoezi zima la kukusanya maoni ya
mtu mmoja mmoja lilivyofanyika na kisha akaeleza kuwa, tume hiyo
inaendelea na zoezi hilo kwa kukutana na makundi maalum sambamba na mtu
mmoja mmoja kufuatia umuhimu wa hoja ambazo tume inakutana nazo na hivyo
kuhitaji ufafanuzi.
Katika muktadha huo, Jaji
Warioba sambamba na kumpa fursa ya kuchangia maoni yake mengine
anayopenda alimtaka Mheshimiwa Makamu wa Rais kujikita zaidi katika
suala la Muungano kufuatia yeye kuwa na uzoefu wa kiuongozi katika
serikali zote mbili yaani ya Muungano sambamba na ile ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Akizungumzia suala la Muungano Makamu wa Rais Dkt. Bilal ameieleza Tume kuwa yeye ni muumini wa Muungano wa serikali mbili na kwamba haoni sababu ya kubadili mfumo uliopo kwa kuwa umeipatia tija nchi yetu na kuipambanua kama nchi yenye muungano wa mfano katika dunia.
Akizungumzia suala la Muungano Makamu wa Rais Dkt. Bilal ameieleza Tume kuwa yeye ni muumini wa Muungano wa serikali mbili na kwamba haoni sababu ya kubadili mfumo uliopo kwa kuwa umeipatia tija nchi yetu na kuipambanua kama nchi yenye muungano wa mfano katika dunia.
Pia alifafanua kuwa mfumo wa serikali mbili
umesaidia kujenga na kudumisha udugu, amani na utulivu baina ya
wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani kwa kipindi cha miaka 49 sasa.
Tanzania imechangia kitu kikubwa
katika historia, kudumisha Muungano wa mfumo wa serikali mbili kati ya
nchi mbili, kubwa na ndogo, jambo ambalo kwa nchi nyingine za Afrika
wameshindwa. Kumekuwepo na nchi nyingi ambazo ziliungana na kushindwa
kudumu kama tulivyo sisi. Hatuna haja ya kujifunza mfumo mpya wakati
tulionao umeweza kudumu, « alisema.
Katika ujumbe wa tume uliofika kuchukua maoni ya Mheshimiwa Makamu wa Rais ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Profesa wa Sheria Palamagamba Kabudi, Ndugu Simai Said, Ndugu Assa Rashid, Ndugu Sasmir Kyuki, Ndugu Salum Athuman, Ndugu Juma Mzalau na Mratibu wa Tume hiyo Ndugu Ramadhan Kailima.
Katika ujumbe wa tume uliofika kuchukua maoni ya Mheshimiwa Makamu wa Rais ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Profesa wa Sheria Palamagamba Kabudi, Ndugu Simai Said, Ndugu Assa Rashid, Ndugu Sasmir Kyuki, Ndugu Salum Athuman, Ndugu Juma Mzalau na Mratibu wa Tume hiyo Ndugu Ramadhan Kailima.
Short URL:
http://www.thehabari.com/?p=27917


