Jeshi la Polisi nchini
limewakamata zaidi ya wasichana 22 katika eneo la Mwananyamala karibu na geti
la hospitali ya Mwananyamala akiwemo mama mtu mzima anayekadiliwa kuwa na umri
wa miaka 70 ambaye alikuwa anamiliki jumba lenye zaidi ya vyumba 40 ambalo hutumika
kufanyia ukahaba maarufu kama danguro.
![]() |
| Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Kamanda Charles Kenyela akizungumza na waandishi wa habari |
Akitoa taarifa leo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Kamanda Charles Kenyela, amesema
kuwa, wanashukuru wananchi ambao wameweza kutoa ushirikiano wa kukamatwa kwa
wasichana hao ambao walikuwa wakifanya biashara ya ukahaba katika maeneo hayo
kwa muda mrefu.
Mashuhuda wa tukio hilo, wamesema
kuwa, wanalishukuru sana Jeshi Polisi kwa kuweza kuwakamata wasichana hao ambao
wamekuwa wakifanya biashara hiyo ya ukahaba kwa muda mrefu.
Aidha mashuhuda hao wamesema kuwa, wasichana hao walikuwa wanafanya biashara hiyo kwa bei ya shilingi 2000, 3000 kwa muda mfupi (short time) na wateja wao ni vijana, akina baba pamoja na vijana ambao huwa wanabarehe kwa vile hawa huwa hawajui mapenzi huko huenda kufundishwa

