KLABU YA WANAHABARI MKOA WA IRINGA KUZINDUA IPC VICOBA JUMAMOSI

 wanahabari  mkoa  wa  Iringa  wakiwa katika  ofisi ya klabu ya  waandishi  wa habari mkoa wa Iringa (IPC) leo wakati wa kikao chao cha  kuelezea lengo la kufanyika kwa mkutano wa wadau  wa habari siku ya jumamosi  wiki hii pamoja na  kuzindua rasmi IPC VICOBA ili  kuwasaidia  wanachama  wake kukopa  fedha za maendeleo
 katibu  mtendaji  wa IPC  Frank Leonard akionesha katiba ya IPC VICOBA ambayo itazinduliwa rasmi siku ya jumamosi  wiki  hii
 
 Na Francis Godwin
Klabu  ya  wanahabari  mkoa  wa Iringa (IPC) inataraji kufanya mkutano mkubwa wa  wadau  wa habari  mkoa  wa Iringa  ikiwa ni pamoja na  kuzindua rasmi asasi ya  mikopo ya IPC VICOBA itakayowawezasha  wanahabari  mkoani Iringa  kukopa  fedha  za kuanzisha miradi ya kimaendeleo ya  kujenga nyumba pamoja na kununua  vifaa vya kazi.

Katibu mtendaji  wa IPC Frank Leonard  akizungumza na  wanahabari leo katika  ofisi ya IPC amesema  kuwa lengo la mkutano  huo ni  kupokea  changamoto mbali mbali za wadau juu  wa wanahabari mkoa  wa Iringa pamoja na kuzindua  rasmi taasisi hiyo ya mikopo  kwa wanahabari ya  IPC VICOBA .


Hivyo  alisema katika  mkutano  huo  wa wadau ambao  pia utatanguliwa na mdahalo   uliaandaliwa na asasi  za kiraia ya ISICO mkoa  wa Iringa kwa ajili ya  kujadili suala  zima la mabadiliko tabia nchi  utafanyika kwenye ukumbi  wa Hinglands mjini Iringa.


Hivyo  amewataka  wanahabari  mkoa  wa Iringa na  wadau  wa habari  kujitokeza kwa  wingi katika mkutano na mdahalo  huo  ambapo mdahalo utaanza mida ya saa 5 asubuhi na kumalizika muda wa saa 8 mchana na baada ya hapo katika ukumbi huo utaendelea mkutano  huo  wa wadau  wa vyombo vya habari  pamoja na uzinduzi  wa IPC VICOBA .


Leonard  amesema  kuwa  viongozi mbali mbali wa vyama  vya siasa na  serikali  wamealikwa katika siku hiyo  kufika kwenye mkutano  huo wa wadau  wa habari.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo