KIBAKA APOKEA MKONG'OTO AKIDAIWA KUWATEKA WATOTO MOROGORO


 Jamaa huyu alimnyanyua juu kibaka huyo kishia kumtupa chini 
                 Wanachi hao wakimgombea kibaka huyo kama mpira wa kona
                                               mkong'oto ukishika kasi

 Kibaka huyo akiendela kupokea kichapo kutoka kwa wnanachi hao wenye hasira
          Jamaa mwenye kofia akimpiga kibaka huyo na kitu chenye ncha kali

 Mwananchi huyu mwenye kofia aliamua kuingilia kati na kumuokoa kibaka huyo asiendele kupokea mkong'oto kutoka kwa wananachi hao
Msamaria mwema huyo aliondoka na kibaka huyo baada ya kufanikiwa kumpora kwenye kundi kubwa la wananchi ambao walikuwa na dhamira ya kutoa roho ya kibaka huyo.

KIJANA mmoja anayesadikiwa kuwa ni kibaka mchana huu amenusulika kifo baada ya kupokea kicha kikali kutoka kwa wnanachi wenye hasira wakimshutumu  kuiba watoto wadogo na kwenda nao  mto  Morogoro eneo la daraja la Shani na kuwafanyia vitendo vya kihuni. 
  
Akizungumza na Mtandao huu mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Juma Athuman alidai kwamba kijana huyo anakawaida ya kuwateka watoto wadogo hasa wa shule na kuwapeleka chini ya daraja hilo na kuwafanyia vitendo vya kihuni.

" kwa kipindi kirefu tulikuwa tukimsaka kibaka huyu ambaye anatabia ya kuwateka watoto wa dogo na kuwapeleka mto wa Morogoro chini ya daraja la Shani muda huu tumemfuma akiwa chini ya daraja hilo ma mtoto mdogo ndipo tulipomfulumusha na kumkata eneo hili la kituo cha mafuta jirani na daraja hili la Shani"alisema Bw Athuman.. 
 
Katika hatu nyingine mwananchi mmoja alijitosa na kumnyakua kibaka huyo kutoka mikononi mwa kundi la wananchi hao na kumpeleka kituo kikuu cha polisi kilichopo jirani na eneo hilo la Shani Snem


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo