| MKUU WA MKOA MBEYA ABAS KANDORO AKIONGEA NA WAHESHIMIWA MADIWANI HIVI KARIBUNI |
| MKUU WA WILAYA MBEYA NORMAN SIGALLA AKIWA NA MKURUGENZI WA JIJI LA MBEYA IDDI WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA |
| WAHESHIMIWA MADIWANI |
HALMASHAURI ya jiji la Mbeya
imeshauriwa kumaliza mgogoro kati
yake na wakazi wa eneo la Sokomatola kwa kuruhusu wakazi hao kufanya
mazungumzo
na wafanyabiashara wakubwa wao wenyewe ili waweze kukubaliana na
kuuziana
nyumba.
Kwa muda mrefu halmashauri imekuwa
ikilumbana na wakazi wa eneo
hilo ambapo ilitaka kuwahamisha na kisha ichukue ilichukue na kugawa
viwanja upya
kwa watu walio na uwezo wa kujenga maghorofa lengo likiwa ni
kupendezesha mji.
Hali hiyo inatokana na nyumba nyingi zilizopo katika eneo la Sokomatola
kuwa za
kizamani na zilizochakaa hali isiyoendana na madhari ya kisasa yaliyopo
kwenye
kituo cha mikutano cha Mkapa cha halmashauri ya jiji la Mbeya kilichopo
maeneo
hayo. Lakini Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameshauri halmashauri
kuwaruhusu wamiliki wa nyumba katika eneo hilo kufanya maamuzi wao
wenyewe kwa
kukubaliana na watu walio na uwezo wa kujenga magorofa na si
kuwaingilia.
“Tumeona mahala kwingi wafanyabiashara au wawekezaji wakubwa wanawafuata
watu
walio na viwanja na kufanya mazungumzo nao na wanakubaliana
vizuri.Wengine
wanawajengea nyumba mbali kisha wanawaachia viwanja ama wanakubaliana
ikijengwa
ghorofa huyu amiliki vyumba kadhaa na mwenzake vinavyobaki”.
“Halmashauri
isiingilie makazi ya watu.Mnadumaza eneo la Sokomatola.Na mnatudanganya
kusema
ninyi mtalinunua kasha muuze viwanja upya pesa hamna mtazitoa wapi.”
Kandoro
pia alishauri halmashauri kufanya mazungumzo na kituo cha utafiti wa
kilimo cha
Uyole jijini hapa ili ili iweze kupewa eneo la mbele lililo pembezoni
mwa
barabara ili litumike kwa ujenzi wa makazi badala ya kilimo kama
linavyotumika
hivi sasa. Alisema ili kuwa na mji wenye mwonekano mzuri ni vema
halmashauri
ikajipanga na kuhakikisha hakuna vichaka katikati ya mji badala yake
iwezeshe
wakazi kupata viwanja kwenye maeneo yaliyo wazi na kujenga
Habari na Mbeyayetu blog