CWT IMEITAKA SERIKALI KUANZA MCHAKATO WA KUWAPANDISHA WALIMU MADARAJA

 
Baraza Kuu la Chama cha Walimu nchini CWT limeitaka Serikali kuanza mchakato wa kuwapandisha Walimu madaraja, sambamba na kulipa malimbikizo ya Mishahara yenye thamani ya zaidi ya Shilinghi Bilioni 20 kufikia mwezi marchi Mwaka huu.

Rais wa CWT,GATIAN MUKOBA amesema kuwa mapendekezo hayo yanafuatia kikao cha kamati hiyo kilichomalizioka hivi karibuni mjini Dodoma, na kubainisha kuwa kikao hicho kwa kauli moja kimeitaka Serikali kuhakikisha inawapandisha madaraja Walimu zaidi ya 60,000 waliostahili kupandishwa kuanzia mwezi Julai mwaka 2012.

MUKOBA amesema Baraza hilo linashangazwa na hatua ambazo Serikali inashindwa kuchukua dhidi ya Walimu hao, wakati tayari Bunge kupitia bajeti ya Mwaka 2012-2013 lilishapitisha fedha za kuwapandishia madaraja sambamba na kutoa idhini ya kulipwa kwa malimbikizo ya mishahara hiyo.

Julai 30 mwaka 2012 Walimu nchini waliingia kwenye mgomo wakiwa na lengo la kuishinikiza Serikali kutatua baadhi ya kero zao mgomo ambao ulielezwa kuwaathiri wanafuzni mbalimbali kitaaluma.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo