![]() |
| Michael Houston. |
Kaka wa Whitney Houston amesema
yeye ndiye wa kulaumiwa kwa kumuingiza mwimbaji huyo kwenye matumizi ya
dawa za kulevya kama cocaine katika miaka ya 1980 … na sio Bobby Brown …
na juzi usiku alikuja akiwa nadhifu mbele ya Oprah.
Michael Houston aliketi chini akiwa na mama yake, Cissy na kuweka bayana uthubutu wake katika "Oprah's Next Chapter" … akikiri kwamba alikuwa mtu wa kwanza kutumia dawa za kulevya na Whitney.
Michael anasema anajihisi mwenye hatia mno kwa kifo cha Whitney -- lakini anasema hakufahamu jinsi gani dawa za kulevya zingeweza kuwa hatari hivyo pale mwanzoni alipomletea Whitney hadi mlangoni … akafafanua: "Unaelewa kwa wakati huo … miaka ya 1980 … ilikuwa ikiruhusiwa."
Michael anaongeza: "Inauma sana … Najihisi kuwajibika kwa kuacha iendelee kwa kipindi kirefu hivi."
Whitney alifariki mjini Beverly Hills Februari mwaka jana baada ya kutumia mseto wa dawa za kulevya uliojumuisha cocaine, Xanax na bangi.
