CHADEMA IMETANGAZA RATIBA YA CHAGUZI ZAKE

 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimetangaza ratiba ya Chaguzi zake ndani ya chama hicho,chaguzi ambazo zinatarajiwa kuanza mapema mwezi April hadi Septemba kwa ngazi za matawi kata,majimbo pamoja na kanda.

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama hicho JOHN MNYIKA, amesema tayari maandalizi yote kwa ajili ya Chaguzi hizo yamekamilika na kubanisha kuwa CHADEMA kimejipanga kuzitumia vizuri chaguzi hizo, ili kuboresha mazingira ya Chaguzi za ngazi ya Kitaifa zinazotarajiwa kuanza Mwezi Novemba hadi Disemba nchini kote.

Katika hatua nyingine Baraza kuu la Chama hicho ambalo limemaliza Mkutano wake Siku ya jana, limetangaza kuanza rasmi kwa kampeni za kuhamasisha wananchi juu ya kutambua haki na wajibu wao wa kumiliki rasilimali na maliasili mbalimbali zilizopo nchini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo