![]() |
| Mandhari ya mji wa Dodoma. |
Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Habbi Gunze alisema hayo jana katika Mkutano wake na waandishi wa habari.
Alisema
maandalizi ya kuzima mitambo ya utangazaji wa televisheni katika Mkoa wa
Dodoma, yamekamilika kwa kushirikisha wadau wa sekta ya utangazaji
Januari 31, mwaka huu saa sita usiku.
Gunze
alisema elimu kwa umma kupitia mbinu mbalimbali kuhusu mchakato wa
kuhamia katika mfumo wa utangazaji wa digitali, imekuwa ikitolewa kwa
kiwango cha kuridhisha ambapo matangazo ya digitali yanawafikia watu
asilimia zaidi ya 20 kati ya watu asilimia 24 wanaopata matangazo ya
televisheni ya analojia.
Alisema
Serikali iliweka ratiba ya uzimaji mitambo ya analojia, ambapo katika
Mkoa wa Dar es Salaam ilizimwa Desemba 31, mwaka jana na Dodoma na
Tanga mitambo itazimwa Januari 31, mwaka huu.
Katika
Jiji la Mwanza mitambo hiyo itazimwa Februari 28, Moshi na Arusha
mitambo itazimwa Machi 31, mwaka huu na Mkoa wa Mbeya mitambo hiyo
itazimwa Aprili 30, mwaka huu.
Alisema mabadiliko hayo hayahusu matangazo kwa njia ya utangazi wa satelaiti, nyaya na redio.
