![]() |
| Penny akiwa kashikilia moyo wake kwa mikono yake mwenyewe baada ya upasuaji. |
Mgonjwa aliyepandikizwa kiungo
amepigwa picha akiwa kashikilia moyo wake mwenyewe kwa mikono yake baada
ya kunusurika kufa kwa saratani na viungo kushindwa kufanya kazi.
Pamoja na kufichwa sehemu kubwa ya uso wake kwa kofia maalumu ya matibabu, macho ya Penny yanaonekana bayana huku moyo wake mpya ukidunda kifuani mwake na akiwa amebeba moyo wake wa zamani kwa mara yake ya mwisho kufuatia mafanikio ya upasuaji aliofanyiwa.
Rafiki wa Penny, Kelsey alituma picha kwenye ukurasa wake wa Imgur akisema: "Penny akiwa amebeba moyo wake mwenyewe. Amenusurika saratani na moyo wake kushindwa kufanya kazi na hakuwahi kukata tamaa."
Kwa mujibu wa maelezo ya Kelsey, madaktari walimruhusu Penny kupiga picha akiwa kabeba moyo wake uliokufa kabla haujachomwa moto.
Akiwa kauzingira wote mikono yake, ameuinua moyo huo karibu na kamera kama vile alikuwa kabeba tuzo.
Sasa picha ya afya njema, anayo picha hii kama ukumbusho wa mateso na kumbusho la jinsi alivyokuwa na bahati kuweza kuwekewa moyo mpya.
