![]() |
Hiki ni choo cha muda cha kwanza cha shule ya msingi Lipangala Ludewa mkoani Njombe kilichobomoka toka mwaka 2004 |
Hiki ni choo cha kisasa ambacho kimejengwa sasa katika shule ya Msingi Lipangala ambacho pia kimeanza kubomoka
Hiki kilikuwa ni choo cha
walimu miaka hiyo kwa sasa shimo jipya linachimbwa mbele ili
kurejesha huduma ya choo kwa walimu
Hii ndilo hali halisi ya choo hiki cha walimu shule ya Msingi Lipangala Ludewa ,kwa sasa hakitumiki
Mbunge Filikunjombe akiagiza choo kujengwa haraka
Na Francis Godwin Blog
WAKATI
serikali kupitia wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ikiendelea
kuweka mikakati ya kuboresha elimu ya awali na msingi ,mbunge wa
jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe asikitishwa na shule ya msingi
Lipangala wilaya Ludewa mkoani Njombe kukosa choo cha walimu na
wanafunzi na kupelekea walimu wa shule hiyo kuendelea kujisaidia
vichakani kwa zaidi ya miaka 5 hivi sasa .
Kutokana
na shule hiyo kukosa vyoo vya wanafunzi na walimu mbunge huyo aagiza
uongozi wa kata
hiyo pamoja na tarafa kuhakikisha wanakamilisha ujenzi vyoo ndani
ya siku 10 kunzia juzi na pindi shule zitakapofungua kuwepo na vyoo
vya uhakika shuleni hapo.
Wakizungumza
katika mkutano wa mbunge Filikunjombe wananchi wa kijiji cha
Lipangala walisema kuwa wnasikitishwa kuona walimu wa shule
hiyo wakikimbi kwenda kujisaidia vichakani huku baadhi yao
wakilazimika kwenda majumbani kwao kupata huduma ya choo jambo ambalo
wmedai ni hatari katika maendeleo ya elimu shuleni
hapo.
Saraha
Edward alisema kuwa mbali ya walimu kuendelea kufundisha shule
hiyo bila ya choo bado wanafunzi wamekuwa wakipata tabu kubwa
kupata huduma ya choo kutokana n vyoo vilivyokuwepo shuleni hapo kuwa
na hali mbaya zaidi.
"Hii
shule yetu ni vema ikafungwa kabisa kwani tunawasiwasi mkubwa watoto
wetu kuja kupatwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na shule kutokuwa
na choo cha uhakika ni kama wanajisaidia porini kwani hivi si vyoo vya
kujivunia kama shule"
Mmoja
kati ya walimu wa shule hiyo ambae hakupenda kutaja jina lake kwa
kuwa si msemaji wa shule hiyo alisema kuwa shule hiyo imekuwa
ikiendeshwa bila choo toka mwaka 2004 ambapo wanafunzi walianza kukosa
choo cha uhakika baada ya kile kilichokuwepo awali kubomoka .
Kutokana
na tatizo hilo la choo cha wanafunzi kubomoka wananchi
walilazimika kujenga choo cha muda ambacho pia hakikuchuku muda
kilibomoka na hivyo kuendelea kushirikiana choo kimoja na walimu kwa
kipindi cha mwaka mmoja na baada ya hao hata choo cha walimu pia
kilibomoka hivyo kukosa choo cha walimu na kulazimika kujenga choo cha
muda ambacho ni hatari pia kwa usalama wa wanafunzi huku walimu wao
wakilazimika kwenda kupata huduma hiyo majumbani kwao ama porini .
Uchunguzi
uliofnywa na mwandishi wa habari hizi shuleni hapo umebaini kuwa
choo cha walimu chenye matundu mawili kilichokuwepo awali kimekuwa
hakitumiki toka mwaka 2005 kutokana na choo hicho kubomoka kutokana
na kujengwa chini ya kiwango pasipo kujengewa saruji huku ardhi ya
eneo hilo ikiwa inaongoza kwa kuwa na unyevu unyevu.
Afisa
tarafa ya Liganga Edward Wayotile alithibitisha madai hayo ya shule
kuendeshwa bila choo na kuwa tayari wameweka mkakati wa kujenga
vyoo katika shule hiyo .
Alisema
kuwa mkakati ni kujenga vyoo vipya vyenye matundu 16 kwa wavulana na
matundu 12 kwa wasichana pamoja na kujenga choo chenye matundu mawili
kwa ajili ya walimu wa shule hiyo.
Kwa
upande wake mbunge wa jimbo hilo la Ludewa Bw Filikunjombe mbali
ya kueleza masikitiko yake juu ya shule hiyo kukosa vyoo bado
aliuagiza uongozi wa kata ,tarafa na wilaya kufika mara moja katika
shule hiyo ili kujenga choo hicho ndani ya siku 11 kuanzia juzi ili
wanafunzi watakapoanza masomo kuwepo kwa huduma ya uhakika ya choo
cha wanafunzi na walimu.
"Haiwezekani shule
kuendeshwa bila vyoo ....sasa naomba viongozi wa elimu wilaya
kushughulikia tatizo hilo mara moja kwani kama tutaacha suala hilo
ni kutoitendea haki elimu ya watoto wetu"
Mbunge
Filikunjombe pia alikabidhi msaada wa bati 50 kwa diwani wa kata
hiyo kwa ajili ya ukamilishaji wa darasa la awali katika shule hiyo
huku akimuagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya
Ludewa kutoa fedha katika mfuko wa maafa kwa ajili ya ujenzi wa vyoo
kwenye shule hiyo.
Wakati
huo huo mbunge huyo aliwataka wazizi wenye watoto waliofaulu
kujiunga na elimu ya sekondari mwakani kuhakikisha wanafanya
maandalizi mapema na kutotumia fedha zote katika sherehe za kufunga
mwaka na kuacha kutenga fedha kwa ajili ya kusomesha watoto
sekondari.