
Mwaka 2012 tutaukumbuka kwa mengi
yapo mema na mabaya. Naomba nikuombe radhi wewe kwa lolote ambalo
niliwahi kukukosea, nawe kama ulinikosea sina tatizo nawe tangu sasa.
Pia naomba nitoe shukrani zangu kwa wote waliohusika katika mafanikio
yangu ya kimuziki. Naamini wengi mlikuwa mstari wa mbele katika
kunishauri, kunipongeza na hata kunikosoa nilipokosea.
Shukrani nyingi ziwafikie radio
presenter, Dj's, Radio na TV zote Tanzania na Afrika naamini bila nyinyi
kuzicheza nyimbo zangu basi nisingefika hapa.
Waandaaji wa magazeti mlikuwa mstari
wa mbele katika kuona nafika mbali kwa kuandika habari zangu na kufika
hata vjijini. Nachukua fursa kuwashukuru pia. Blogs mbalimbali. Mlikuwa
mstari wa mbele kwa kuandika habari na kupost hata baadhi ya show zangu
ambazo mmenipa heshima ya kufika mbali zaidi na kusikika hata nje ya
nchi mchango wenu ni mkubwa japo siwezi kuwataja wote.
Pia Requester wa media sina cha
kuwalipa nawashkuru sana sana na nitabaki kuwaheshmu kwani mmetoa
mchango mkubwa sana kwa kuomba nyimbo zangu media na zikachezwa na amini
ni mchango mkubwa sana katika game hasa kwetu wasanii nitabaki
kuwaheshimu na kuwathamini siku zote. Bila kuwasahau wasanii wenzangu
walikuwa nami bega kwa bega kunishauri na kunisaidia kwa chochote. Pia
ma dj wa club mbalimbali, mmekuwa chachu ya mziki wangu pale mlipoonesha
ushirikiann wenu kwangu. Pia Waandaaji wa (show) matamasha madogo na
makubwa nawashukuru sana kwa kuniamini na kukubali kufanya kazi na
pamoja nami.

Nawatakia mwaka mpya.
Ni mimi. Dayna Nyange (mkali wao)