
Rais
wa Makapera Tanzania, Issa Kwisa Mwaifuge, leo ameamua kuwageuka
wafuasi wake rasmi na kuvunja katiba ya kundi lake na kuamua kuuaga
ukapera rasmi na kumuoa Binti mrembo aliyewahi kushiriki shindano kubwa
la Miss Tanzania, 2004, Verdiana Kamugisha, ambao kwa pamoja wameamua
kufunga ndoa yao katika Kanisa la Lutheran lililopo mitaa ya Sinza
jijini Dar es Salaam. Sherehe ya ndoa yao ilifanyoka katika Ukumbi wa
Msasani Makuti. Picha na www.sufianimafoto.blogspot.com