Na Elizabeth
John
NYOTA wa muziki
wa kizazi kipya
nchini, Omary Faraji ‘Ommy Dimpoz’ ameachia kibao chake kipya
kinachokwenda kwa
jina la ‘Koikoi’.
Akizungumza na
Habari Mseto jijini
Dar es Salaam, Ommy amesema anaamini wimbo huo utapokelewa vizuri na
mashabiki
wake kutokana na mashairi ya wimbo huo ni ya kuburudisha jamii
inayomzunguka.
“Namshukuru
mungu kazi zangu zote
zinapokelewa vizuri na mashabiki wangu, hivyo nimejipanga kutoa burudani
iliyokwenda shule kwa kutumia kipaji changu ikiwa ni njia moja wapo ya
kujivutia
mashabiki wa kutosha,” amesema Ommy Dimpoz.
Amesema
anawaomba mashabiki na
wapenzi wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea video ya
kazi hiyo
ambayo anatarajia kwenda kuitengeneza nje ya nchi.
Ommy Dimpoz
kwasasa anatamba na
nyimbo zake kama, Nai nai na Baadae ambazo zilimtambulisha na
zinaendelea
kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa bongo fleva.