Marehemu Eustace Nyaruganda
Na Francis Godwin
WANAHARAKATI wa waangaliza wa haki za binadamu kutoka nchi mbali
mbali za Afrika Mashariki ambao wanaendelea na mafunzo ya uangalizi
wa haki za binadamu jijini Daresalaam wameeleza kusikitishwa na taarifa
za kifo cha mwanaharakati mwenzao haki za binadamu wa mkoa wa Mara
Eustace Nyaruganda 45 aliyekutwa amekufa katika nyumba moja ya kulala
wageni(Guest) mjini hapo.
Mbali ya kusikitishwa na mauwaji ya mwanaharakati mwezao huyo pia
wameeleza kusikitishwa na kitendo cha kinyama alichotendewa mwandishi
wa habari wa magazeti ya Free Media Shaban Matutu aliyepigwa risasi
na watu wanaosadikika kuwa ni askari polisi matukio waliyodai kuwa
ni kinyume na haki za binadamu .
Wakizungumza leo katika mahojiano maalum na kipindi cha gali la
matangazo la Radio Nuru Fm ya mkoani Iringa kutoka Hotel ya White
Sands Kunduji jijini hapa wanaharakati hao akiwemo mwanaharakati
aliyekuwa akifanya kazi na marehemu huyo mkoani Mara Angela Benedict na
afisa shughuli wa shirika la ABC Foundation,Andreas Migiro walisema
kuwa wamepokea kwa masikitiko makubwa juu ya taarifa za msiba wa
mkurugenzi wake aliyekuwa amekufa asubuhi ya leo ikiwa ni baada ya
kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa siku kadhaa .
Wakati Angela akidai kuwa taarifa
ya kifo hicho imemshitua zaidi na kuomba uchunguzi wa kina wa
kifo cha mwenzao huyo kutolewa bado kwa upande wake Migiro alisema
kuwa alipewa taarifa kuwa mkurugenzi wao alikutwajana asubuhi akiwa
amekufa katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Savana
iliyoko katika mtaa wabenki mjini Bunda.
Akizungumzia kifo hicho cha mwanaharakati huyo,mratibu wa mtandao wa
kutetea watetezi wa haki za binadamu nchini,Tanzania Human Right
Defenders Coalitions, Onesmo ole Ngulumwa amesema kuwa mtandao umepokea
kwa masikitiko makubwa sana juu ya kifo hicho na kwamba ni pigo kwa
watetezi wa haki za binadamu kwani alimfahamu kwa karibu sana marehemu
na kuwa kituo chake kitatoa taarifa kamili juu ya kifo hicho
mapema leo .
Mratibu huyo alisema kuwa anatarajia leo kuongea na vyombo vya habari
juu ya tukio la kifo hicho cha mwanaharakati ambapo pia amewaomba ndugu
na jamaa wa karibu na marehemu ikiwa ni pamoja na jeshi la polisi
kuhakikisha wanasimamia kwa karibu ili mwili wake uweze kufanyiwa
uchunguzi wa kina na dakitari kabla haujazikwa.
Hata hivyo baadhi ya wanaharakati wanaohudhilia mafunzo hayo wameonyesha
kusikitishwa sana na mazingira ya kifo hicho ambapo wamesema kuwa hivi
sasa maisha ya wanaharakati yako hatalini hivyo ni lazima waishi kwa
tahadhali sana.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalum Mwakyoma alipopigiwa simu alisema
hana taarifa na tukio hilo na akasema apigiwe simu mkuu wa polisi wa
wilaya hiyo ambapo yeye pia alisema yuko safari na kuelekeza kwa mkuu wa
upelelezi wa wilaya ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba wanaendelea na upelelezi zaidi.
Wakati huo huo mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini Tanzania
Absalom Kibanda akieleza kusikitishwa na vitendo vya uvunjifu wa amani
vinavyoendelea kufanywa na jeshi la polisi nchini na kuwa itafika
wakati wanahabari nchini watahofia kufanya kazi na jeshi la polisi
kutokana na vitendo hivyo vinavyoendelea kufanyiaka na kuona kama polisi
ni maja ya maeneo ya hatari kwa wanahabari nchini .
Kibanda alidai kuwa anashindwa kujua sababu ya jeshi la polisi
kumpiga risasi mwandishi wa gazeti la Tanzania daima Bw Matutu akiwa
nyumbani kwake na kudai kuwa tukio hilo limefanyika kwa bahati mbaya
na kuwa wao walikuwa wakimsaka mtuhumiwa wao wa kike na badala yake
kumpiga mwanahabari huyo.