Na Abdulaziz,Lindi
UPEPO mkali uliombatana na mvua kubwa umeziathiri baadhi ya nyumba
huku shule ya sekondari ya Mnacho wilayani Ruangwa ikipata athari kwa
kiasi kikubwa baada ya madarasa sita kuezuliwa mabati na baadhi ya
wanakijiji kupata majeraha na kusababisha wakazi wengine kukosa mahali
pa kuishi.
Upepo huo uliotokea jana ni mfufulizo wa matukio hayo kwa vijiji vya
kata hiyo ambapo awali mwanzoni mwa mwaka huu uliezua madarasa mawili
ya shule hiyo.
Akitoa taarifa ya maafa hayo ya jana katika kikao cha Baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya Ruangwa leo, Mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya hiyo,Bw Reubern Mfune alieleza kuwa Kufuatia
kuwepo kwa tukio hilo lilitokea jana jioni Ofisi yake ilifika eneo la
tukio akiwemo na mkuu wa wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzira na
tayari wamepelekwa wataalamu kutathimini athari hizo ili shule hiyo
inayotarajiwa kuanza muhula jan 14 Halmashauri yake itashirikiana na
ofisi ya mkuu wa wilaya kuhakikisha hali ya shule inakamilishwa.
Aidha Mkurugenzi alibainisha katika kikao hicho cha baraza la madiwani kuwa
Katika maafa hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yaliathiri shule hiyo bado
ni changamoto katika Halmashauri yake kufuatia kupangawa kupokea
wanafunzi 92 wa kidato cha kwanza na inatarajiwa kufunguliwa jan
14,2013
Katika maafa hayo Mtu mmoja alijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini