Mkuu wa
kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi
Marison Mwakyoma akiongea na madereva wa Boda Boda kwenye mkutano
uliofanyika katika uwanja wa wazi uliopo kata ya kimandolu jijini
Arusha.(Picha na mahmoud ahmad Arusha)
Mkuu
huyo wa Usalama barabarani amesema ameanzisha kampeni hiyo ili kila
mmoja apate mafunzo yake kupitia chuo hali ambayo itasaidia kupunguza
ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa.
Mkutano
huo uliohudhuriwa na Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi
Gilles Muroto, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi toka Dawati la Jinsia na
Watoto, Maria Maswa, Polisi tarafa, viongozi wa tarafa ya Suye, kata,
mitaa na madereva wapatao 100 ulitawaliwa na
makofi ya pongezi pamoja na vifijo kutoka kwa madeva hao baada ya Mkuu
huyo wa Usalama Barabarani kuwaahidi kuwa kama wangekuwa tayari hata
siku ya pili yake (jana) wangeweza kuanza darasa.
Alimalizia
kwa kuwaasa madereva hao kutojichukulia sheria mkononi pindi mwenzao
anapogongwa na gari kwani vitendo hivyo vinaweza kuwagharimu badala yake
aliwataka wafanye mambo manne muhimu; kwanza kuandika namba ya gari
iliyosababisha ajali, kuielewa mahali ajali ilipotokea, kutoa taarifa
polisi na mwisho kumwahisha mwenzao hospitali.
Programu
ya mafunzo kwa waendesha pikipiki mkoani hapa ilianza rasmi mwezi
Agosti mwaka huu baada ya kufunguliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas kutokana na kuwepo
kwa ongezeko kubwa la ajali.
Hadi sasa waendesha boda boda wapatao 900
kutoka wilaya
za Arusha mjini, Arumeru na Monduli wamekwisha pata mafunzo ya udereva
toka vyuo mbalimbali vilivyopo mkoani hapa.
|