ZAIDI YA MILIONI 78 KUKARABATI BARABARA ZA MITAA KATA YA IWAWA WILAYANI MAKETE


Zaidi ya shilingi milioni sabini na nane zimetengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Makete kwa ajili ya ukarabati wa barabara za mitaa katika kata ya Iwawa

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Afisa Mtendaji wa Kata ya Iwawa  Bw.Suleimani Kiwone amesema kuwa mpango huo utanufaisha wananchi wa Wilayani Makete kulingana na serikali inavyowajali.

Hata hivyo Bw. Kiwone amewaomba wenye vifaa vifaa vya ujenzi kandokando ya barabara hizo kuvitoa mara moja kwani ukarabati wa barabara hizo umekwisha kuanza rasmi.

Aidha Bw. Kiwone amezitaja changamoto wanazokumbana nazo kipindi cha ujenzi wa awali ambazo ni wananchi kutokuthamini miundombinu hiyo kwa kutupa takataka ovyo na kusababisha kuziba kwa mifereji inayopitisha maji.

“Hebu fikiria ndugu mwandishi barabara zinajengwa kwa gharama kubwa namna hii halafu wengine wanaleta vifaa vya ujenzi kama mchanga na mawe halafu wanaviweka kando mwa barabara halafu wanachukua muda mrefu bila ujenzi wowote kufanyika, mvua zinanyesha maji yanakosa mwelekeo yanaanza kuharibu barabara kwa kuwa mifereji imeziba” alisema Kiwone

Katika hatua nyingine Diwani wa kata ya Iwawa Mh. Benjamini Mahenge amesema kuwa mwananchi yeyote atayeharibu barabara hizo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake amesema hayo wakati wa makabidhiano ya fedha za kukarabati barabara hizo.

Ameseme hakuna atakayeonewa huruma kwani barabara hizo mara nyingi zimekuwa zikikarabatiwa kutokana na makosa yale yale ya miaka yote

Na Hadija Sanga.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo