Baada ya kupata usumbufu mkubwa wa maji kwa kipindi muda mrefu Wananchi wa kijiji cha Maleutsi wilayani Makete hivi sasa tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi
Akizungumza na wanahabari mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Reuben Mbilinyi amesema ujenzi wa mradi wa maji ulianzakutekelezwa mwezi septemba 2012 ambapo kwa sasa chanzo cha kuhifadhia maji kimeshakamilika ikiwa imegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mbili.
Mwenyekiti huyo amesema kwamba fedha hizo zimetolewa kwa nguvu zamichango ya wananchi ikiwa kila mmoja amekuwa akichangia kiasi cha shilingi elfu kumi na saba na mia tano na michango hiyo imekuwa ikitolewa bila usumbufu mkubwa kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho.
Bw. Mbilinyi ameongeza kwamba wamekuwa wakikabiliana na tatizo kubwa la kukosa maji kwa kipindi cha muda mrefu ambapo maji yanatoka katika kijiji jirani cha Ugabwa kutokana na usumbufu huo wananchi wengi hulazimika kutumia maji ya mtoni
Hata hivyo amesema kwa sasa wanaendelea na uchimbaji wa mtaro kwa ajili ya kupitisha bomba la maji na amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu
Na Furahisha Nundu.