WANAMAKETE WASHAURIWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KUSOMA MASOMO YA UFUNDI

Na Hadija Sanga, Makete

Chuo kinachotoa mafunzo ya elimu ya ufundi ikiwemo ushonaji, useremala na ujeanzi wa nyumba cha Shukurani  Centre kilichopo Ndulamo wilayani Makete kimewataka wazazi na walezi kuwapeleka  watoto wao kupata elimu ya ufundi huo.

Akizungumza na mtandao huu chuoni hapo Mkuu wa chuo hicho Bw. Aizaki Mwihumbo amesema kuwa chuo hicho kinatoa huduma mbalimbali kwa wanafunzi hao ambazo hutolewa bila gharama zozote.

Bw.Mwihumbo amesema kuwa chuo hicho kimesajiliwa na Veta pia kinatoa mafunzo kwa wanafunzi walio na zaidi ya umri wa miaka kumi na tatu ambapo mpaka sasa chuo hicho kina jumla ya wanafunzi sitini na saba.

Amesema kwa sasa maendeleo ya chuo hicho ni mazuri na masomo ya nyongeza yanayotolewa chuoni hapo ya kiingereza, stadi za maisha, hisabati, ujasiriamali pamoja na dini huwafanya wanafunzi kuwa na uelewa zaidi katika soko la ajira.

“Unajua vyuo vingi huwa vinafundisha yale masomo ya ufundi tu, lakini hapa sisi tunafundisha na mengine ya ziada kama kiingereza kwa kuwa tunaamini wanafunzi wetu wanaweza hata kuajiriwa kimataifa sasa kama hata kiingereza hawajui unadhani itakuwaje” alisema mkuu huyo

Hata hivyo Bw.Mwihumbo ameiomba serikali itambue kuwa kuna kituo kinachosaidia watoto hao na pia amewaomba wazazi wa wanafunzi hao kutoa ushirikiano kwa pamoja katika kuwalea wanafunzi waliopo chuoni hapo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo