MHARIRI WA GAZETI LA BUSINESS TIMES APIGWA RISASI

 

Mnaku Mbani Lukanga (Mhariri wa gazeti la Business Times ) akiwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili leo asubuhi alipohamishwa kutoka hospitali ya Temeke alikolazwa jana mara baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi hapo jana usiku katika mtaa wa Lugoda akiwa anaelekea nyumbani kwake Mbagala usiku wa saa mbili jioni.

Katika tukio hilo, alikuwa na abiria wenzake 6 ambao nao walipigwa risasi.

Baadhi yao walitolewa risasi na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Mnaku alipigwa risasi juu yo mdomo na risasi hiyo kutokea kwenye shavu lake la kushoto. Bado yuko chini ya uangalizi wa madaktari.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo