SERIKALI YAWASHANGAA MADIWANI WALIOGOMA KUMCHAGUA MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI


SERIKALI Mkoani Manyara imelaani kitendo kinayofanywa na Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara kuendelea kuahirisha kwa mara ya tatu sasa kwa kutofanyika kwa uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na kusema kuwa ni kufuja fedha za wananchi.

Hayo yamesemwa jana na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw.Claudio Bitageko wakati alipokuwa akizungumza katika kikao cha Baraza la madiwani kama mgeni rasmi kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang’ mkoani humo

Aidha Bitageko aliamua kuhudhuria kikao hicho baada ya kupewa taarifa ya madiwani kukataa kurudia uchaguzi wa makamu mwenyekiti baada ya wagombea wawili wa Chadema na CCM kura kugongana na hivyo upande wa Chadema kuitaka Halmashauri kutofanya uchaguzi zaidi ya kugawa madaraka kwao .

Uchaguzi huo kwa mara ya kwanza ulifanyika septemba 19 mwaka huu ambapo hawakufikia muafaka ya kupiga tiki kwa ajili ya mgombea watakayempigia kura ambapo kiliahirishwa hadi oktoka 3walipopiga kura ambapo kura ziligongana kwa wagombea hao wawili ambao ni Diwani John Bajuta (CCM)kutoka kata yaSimbay aliyepata kura 18 na Diwani Peter Lori(CHADEMA) kata ya Katesh mjini aliyepata kura 18 hali iliyoleta tafrani ndani ya kikao kilichopelekea kuahirishwa kwa kikao hadi octoba 29nacho hakikuweza kuleta suluhu licha ya kuketi kwa zaidi ya masaa manane hali iliyopelekea wananchi waliokuwa wakisubiri kwa shauku kutangwa kwa makamu mwenyekiti kupiga kelele ya kwamba madiwani hao wameshidwa kuchukua uamuzi wenye busara wa kuamua nani awe makamu mwenyekiti licha ya uwepo wa katibu tawala huu.

Kufuatia hali hiyo.Katibu tawala huyo alisema kuendelea kwa malumbano na migongano inayopelekea kuahirishwa kwa vikao vya mara kwa mara ni kufuja fedha za wananchi ambapo husababisha ulegevu katika Halmashauri ya wilaya hiyo amewataka madiwani wanaofanya fujo kuacha tabia hiyo.

Alisema kuwa madiwani hao wanatakiwa waende mbele nasi kuangalia ya nyuma ili kuweza kuwaletea maendeleo mazuri wananchi wao na sio kukaa na kuwaza ni njisni gani wafanye ili kujipatia fedha zinazookana na vikao kama hivyo.

"Msipende kuleta malumbano yasiyokuwa na tija kisa uongozi kufanya hivyo ni kufuja fedha za wananchi ambao wamewatumeni kuja kuwaletea maendeleo"alisema Bitegeko

Naye mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Filex Mabula aliwataka madiwani hao kwenda kwa pamoja na kufuata muda,waheshimiane pamoja na kujaliana katika hiyo ili kuweza kuleta maendeleo pamoja na kusonga mbele.

Aliongeza kuwa madiwani wanatakiwa kufuata kanuni na sheria ili kuweza kusonga mbele katika kuchangia hoja zingine mbalimbali kwaajili ya wananchi wao,wafuate kanuni iendane na sheria inayohusika.

Kwa upande wao baadhi ya madiwani hao kambi ya Chadema walidai ni vyema madiwani wakachukua busara ya kugawa madaraka kwa kuwa mwenyekiti ametokea ChamaCha Mapinduzi basi na Makamu Mwenyekiti aweze kutoka CHADEMA.

walidai kuwa hawatakubali kurudia uchakuzi huo ambao unaonekana kuelekeza zaidi upande wa CCM na hivyo hawatariji kufanya mazmuzi kinyume na wanavyotaka wao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo