RAIS KIKWETE KUZINDUA BARABARA YA MIJINGU-SINGIDA


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya mrisho Kikwete anatarajia kuzindua barabara ya kiwango cha lami kutoka Minjigu hadi singida sambamba na kufanya mikutano wa hadhara katika wilayani za Babati na Hanang’ mkoani Manyara

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi Chiristina Mndeme Akitoa Taarifa hiyo jana wakati akizungumza na madiwani pamoja na viongozi mbalimbali kwenye kikao cha Baraza la madiwani cha Wilaya hiyo

Alisema kuwa Rais atafanya mkutano huo wa hadhara Novemba 4 mwaka huu katika shule ya msingi Katesh B na kuwataka viongozi hao kutumia fursa hiyo kwa kuwaeleza wananchi wao kuhusu ugeni huo.

Mkuu wa wilaya huyo alieleza kuwa wananchi wa wilaya hiyo wanatakiwa kuhamasishwa mapema ili kuweza kuhudhuria mkutano huo wa hadhara nakuweza kumsikiliza Rais Kikwete.

Aliongeza kuwa wamepata fursa fupi kwa kipindi hiki ambapo Rais wakati akiwa wilayani Hanang’ atamwona mwananchi ambaye ni mbunifu wa zana za kilimo kwa kutumia mashine kwaajili ya mazao mbalimbali pamoja na kutembelea vikundi vinavyotengeneza bidhaa za ngozi(asili).

Aidha allisema kuwa kwa Mkoa wa Manyara ni Wilaya mbili tu ambazo ni Wilaya ya Babati na Hanang’ ndizo wilaya zilizoteuliwa kwaajili ya ziara ya Rais Dr Kikwete hivyo wilaya hizo zinatakiwa kutumia fursa hizo vizuri ili kuweza kumsikiliza Rais.

Hata hivyo aliwawataka wakazi wa wilaya ya Hanang’ pamoja na vitongoji vyake kuhudhuria kwa wingi kwenye mkutano huu wa hadhara ili kuweza kutoa kero zao walizokuwa nazo pamoja na kumsikiliza Rais atakachowaeleza.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo