MAANDALIZI YA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA LUDIHANI MAKETE YANAENDELEA VIZURI



Imeelezwa kuwa maandalizi ya ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Ludihani Wilayani Makete bado yanaendelea.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Afisa Mtendaji wa kijiji cha Ludihani Bw.Dakta Jaska Mahenge amesema kuwa eneo kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo tayari limeandaliwa vikiwamo mchanga na mawe.

Bw.Mahenge amesema kuwa wameshindwa kuanza ujenzi huo mara moja kutoka na ramani ya ujenzi wa zahanati iliyotolewa na serikali kuwa kubwa ambapo amesema ujenzi wa ramani ya sasa unakadiriwa kugharimu zaidi ya sh. Milioni 500 hivyo kushindwa kumudu kiasi hicho kwa wakati kulingana na kipato kidogo walicho nacho

Pia ameiomba serikali itambue uwezo mdogo wa kifedha wa wananchi wake na kuwaomba wafadhili mbalimbali wenye uwezo kujitokeza kutoa michango yao ili kufanikisha ujenzi huo.

Hata hivyo Bw. Mahenge ameeleza changamoto ambazo wanakabiliana nazo kuwa ni pamoja na uhaba wa mchanga wa kujengea kutokana na mchanga huo kutoka nje ya kijiji hicho 

Bw.Mahenge anawaomba wananchi kutoa michango kwa manufaa yao na pia kushiriki katika shughuli za kimaendeleo kwani suala la ujenzi wa zahanati ni kwa ajili yao kutokana na umbali wa zahanati wanalio nao kwa sasa.

Na Elicia moshi na Hadija Sanga


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo