Ikiwa zimepita siku chache tangu wakala wa udhibiti wa nishati na maji EWURA kuzuia shehena ya mafuta kusafirishwa nje ya nchi kutokana na uhaba wa mafuta uliopo, bei za mafuta bado ni kubwa wilayani Makete.
Akizungumza na vyombo vya habari muuzaji wa mafuta aina ya diesel na petroli Iwawa mjini Bw. Alex Kyando amesema wamekuwa wakihahangaika kununua mafuta hayo kulingana na uhaba unajitokeza.
Bw.Kyando amesema bei za petrol na diesel zimepanda ikiwa petrol inauzwa kwa shilingi 2500 kwa lita tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa ikiuzwa sh.2400 kwa lita na diesel inauzwa sh 2300 kwa lita moja toka awali.
Ameongeza kuwa wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbaliikiwa ni pamoja na uhaba wa mafuta,usumbufu kutoka kwa wateja na mabadiliko ya bei za mara kwa mara za kushuka na kupanda kwa bidhaa hiyo
Hata hivyo Bw.Kyando amewaomba wafanyabiashara wakubwa wa mafuta kupunguza bei za mafuta ili kupungua kwa tatizo la uhaba wa bidhaa hiyo na usumbufu unaojitokeza katika biashara hiyo.
Na Furahisha Nundu.