USAFIRI WA TRENI DAR WAKOSHA WANANCHI

Kichwa cha treni pamoja na mabehewa sita ya awamu ya kwanza,yakisubiri kufanyiwa majaribio kwa Safari zitazoanzia Station Dar es Salaam Mpaka Ubungo mnamo mwezi wa kumi,majaribia hayo yameongozwa asubuhi ya leo na Naibu Waziri wa Uchukuzi,Mhe. Dk Charles Tizeba(Mb) ambaye alipanda treni hiyo kuanzia Station Dar es Salaam Mpaka Ubungo.Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bil 4.75 kwa ajili ya
ukarabati wa njia,injini na mabehewa.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania(TRL)wakiwa na furaha ndani ya mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio leo abubuhi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(Mb) dirisha la pili kutoka kulia,akiangalia nje wakati wa majaribio ya mabehewa sita kati ya kumi na mbili yatakayofanya safari zake kutoka Station mpaka Ubungo kuanzia mwezi wa Kumi mwaka huu,Treni hizo zitasaidia wananchi katika usafiri jijini Dar es Salaam.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo