Redio zilizopo mikoa mbalimbali hapa nchini zimetakiwa
kuboresha vipindi vyao ili viendelee kuvutia wasikilizaji pamoja na kuzidi
kuwaelimisha zaidi
Rai hiyo imebainika wakati vituo 10 vya redio vinavyofanya
kazi kwa kushirikiana na Johns Hopkins University Centre for Comuunication
Programs (JHU-CCP) vilipokutana hii leo kwenye hoteli ya Top Life iliyopo
mkoani Morogoro
Wakizungumza wakati wa warsha hiyo watangazaji na waandaji
hao wa vipindi wamesema, kudaiwa malipo wakati wa kufanya vipindi ni moja ya
changamoto kubwa wanayokumbana nayo inyopelekea vipindi vyao kupwaya kwa kuwa
hawana fedha za kuwalipa
“Unajua hili ni tatizo kubwa, wataalamu wengi wanadhani tuna
fedha za kuwalipa, lakini wanasahau kuwa wao ni kioo cha jamii pia wanatakiwa
kutusaidia kuwapa ufafanuzi wasikilizji wetu kuhusiana na mada mbalimbali kwani
wao ndio wataalamu wenyewe, lakini pia wananchi nao wanatakiwa kutoa taarifa tu
bila kudai malipo, sisi hatuna hela” alisema Jumanne Juma mtangazaji wa Nuru FM
mkoani Iringa
Vituo kumi vya redio ambavyo ni Nuru FM, Ebony FM, Uplands
FM, Kitulo FM, Bomba FM, Radio Free Africa, Voice Of Tabora, Victoria FM, Uhuru
Fm na Radio One Stereo ni vituo ambavyo vimekuwa vikifanya kazi na JHU-CCP
kutoa elimu kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwemo VVU/UKIMWI ambapo pia kwa
hivi sasa Clouds FM, Times FM na Best FM ni vituo ambavyo vimeongezwa kufanya
kazi pia na shirika hilo
Mafunzo hayo yanalenga kuboresha vipindi hivyo na kuvifanya viwe
bora zaidi na kuzidi kuwavutia wasikilizaji wa redio hizo
