Nawaomba
wananchi na wadau wa sekta binafsi mnaotumia Barabara ya
Kimara-Mavurunza-Bonyokwa muwasiliane na Diwani wa Kimara Pascal Manota
0784954657 awape utaratibu wa kuchangia kuwezesha kukodi grader
kusawazisha na
malori kuweka vifusi kwenye maeneo korofi kwa dharura wakati tukisubiri
matengenezo ya haraka yanayopaswa kufanywa na Serikali kwa kodi zetu;
mimi
tayari nimeshampatia mchango wangu wa shilingi laki mbili kati ya
milioni moja
zinazohitajika, wewe je?
Izingatiwe
kwamba tayari Wizara ya Ujenzi ilishakubali kuihudumia barabara hii na
wiki
chache zilizopita niliandika barua kwa meneja wa TANROADS Mkoa wa Dare
es
Salaam kutaka hatua zake kwa hali mbovu ya barabara hiyo pamoja na kuwa
kero wa
wananchi inamwaibisha Rais Kikwete mbele ya wakazi husika kwa kuwa
alitembelea
mwaka 2010 na kuahidi itajengwa kwa kiwango cha lami.
Aidha,
mwaka 2011 ilifanyiwa matengenezo ya kawaida lakini kwa sasa imeharibika
tena
kufuatia mvua zilizonyesha, hali mbovu ya barabara hiyo inaathiri pia
hatua za
kupunguza msongamano kwenye barabara ya Morogoro wakati huu ujenzi wa
mradi wa
mabasi yaendayo haraka (DART) unapoendelea kwa kuwa barabara hiyo
hutumika kama
njia mbadala kutoka Manispaa ya Kinondoni mpaka Manispaa ya Ilala.
Leo na kesho nitakuwa kwenye mfululizo wa mikutano
ya baraza la madiwani wa jiji hivyo wakati nikiendelea kufuatilia majibu
ya
hatua za haraka za serikali kuwezesha matengenezo makubwa, naomba
utaratibu kwa kushirikiana na diwani na
watendaji kwa ajili ya kuunganisha wananchi wa maeneo husika na wadau
wengine
ili kufanya matengenezo madogo kupunguza kero uendelee.
John
Mnyika (Mb)
10/09/2012