Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Chuo
cha UIinzi (National Defence College) leo Septemba 10, 2012 Kunduchi
jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali
Davis Mwamunyange na kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali
Charles Makalala na kushoto kabisa ni aBalozi wa China nchini Tanzania
Mhe. Lu Younqing. PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mkuu wa Chuo cha
UIinzi (National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala leo
Septemba 10, 2012 baada ya kumkabidhi mfano wa funguo kama ishara ya
kufungua rasmi chuo hicho kilichopo Kunduchi jijini Dar es salaam. Kulia
ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkuu wa Chuo cha UIinzi
(National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala baada ya
kufungua rasmi chuo hicho kilichopo Kunduchi jijini Dar es salaam. Nyuma
yao ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamsi Vuai
Nahodha anayefuatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis
Mwamunyange
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma hotuba yake kufungua rasmi
Chuo cha UIinzi (National Defence College) kilichoko Kunduchi jijini Dar
es salaam, pamoja na kuzindua kozi ya kwanza ya mwaka mmoja. Walioketi
karibu yake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na
Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makalala
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisoma akipozi na wanachuo wa kozi ya kwanza ya
bmwaka mmoja katika Chuo cha UIinzi (National Defence College)
alichofungua rasmi leo Septemba 10, 2012 Kunduchi jijini Dar es salaam.




