Moshi
WAKAZI wa Kibosho
Manushi kata ya Kindi mkoani Kilimanjaro wamelazimika
kukimbia makazi yao kwa kuogopa kamatakamata ya wa polisi maofisa wa shirika la
umeme Tanesco kutokana na wakazi hao kujiingizi umeme kinyume cha sheria.
Kaimu meneja wa
shirika la Tanesco Honest Moshi, alisema hayo jana wakati walipotembelea
nyumba za watu wakazi wa kibosho Manushi ambao wanajiingizia umeme
majumba kwa kutoka kwenye nguzo za umeme.
Moshi alisema
katika nyumba 15 walizotembelea walikuta kuna umeme ambao umeingizwa
kinyemela na kukuta hakuna mtu yoyote katika nyumba hizo
Kaimu huyo
alisema kuwa kibosho ndiko kulikokithiri kwa wizi wa umeme ambapo nyumba
moja inaweza kugawia umeme nyumba nyingine tano kwa kutumia nyaya
nyembamba hali ambayo ni hatari kwa wakazi hao.
“Taarifa za watu
hao tunazo na tutafauatilia mmoja hadi mwingine ili kuweza kuwakamata
wote waliokimbia na kuwafikisha katika vyomba vya sheria”alisema Moshi
Alisema pamoja na
wakazi hao kukimbia wamefanikiwa kukamata watu wawili na kuweza kuwafungulia
mashata ya kuhujumu shirika hilo.
Kaimu huyo
aliwataka wakazi wa kibosho kuendelea kutoa taarifa za watu wanaotumia
umeme kinyume na taratibu za shirika hilo ili waweze kutiwa mbaroni.