SIHA
MADEREVA wa bodaboda wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wamelitaka jeshi la
polisi mkoani hapa kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika na matukio ya
utekaji nyara wa madereva hao ikiwa ni pamoja na kuuwawa kikatili na
kuporwa mali zao jambo ambalo limekuwa likiwakatisha tama kufanya kazi
hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mafunzo ya waendesha bodaboda juu ya kufuta sheria za barabarani ili kuepuka ajili zisizo za lazima,
walisema kuwa kumekuwa na matukio mengi ya utekwaji nyara madereva wa
bodaboda na kuuwawa kikatili kisha kutelekezwa maporini na kupotea katika
mazingira ya kutatanisha.
Walisema jeshi la polisi halina budi kuhakikisha wanaendesha msako mkali
ili kuwabaini watu hao ambao wamekuwa wakifanya vitendo hiyo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kutokana na kwamba vijana wengi wamekuwa wakitegemea kazi hiyo ili kujikwamua kutoka katika vimbi la umasini.
Wakizungumza madereva hao Hamisi Shaban na John Masoy, walisema kuwa
kutokana na ukosefu wa ajira nchini vijana wameamua kuingia katika bishara
hiyo na kuondokana na makundi uvutaji wa madawa ya kulevya pamoja na
makundi ya ujambazi na kwamba pasipo kuchukuliwa hatua za hara za kuthibiti tatizo hilo kuna uwezekano mkubwa wa vijana kurudi katika makundi hao.
Aidha madereva hao wameilalamikia halimashauri hiyo kupandisha gharama za
ushuru hadi kufikia kisia cha shilingi 30,000 kwa mwaka jambo ambalo
walisema ni uonevu kutokana na faida ndogo wanayo ipata kutokana na
biashara hiyo kutokana na kuwepo kwa malipo mengi.
Akijibu malalamiko hayo afisa biasara wa wilaya hiyo Christa Ndosa, alisema
kuwa ushuru huo uliwekwa kwa taratibu na sheria za halmashauri hiyo hivyo
ni vyema wakavumilia ushuru huo mpaka hapo sheria hiyo itakapo fanyiwa
marekebisho.
Kwa upande wake mkuu wa makosa
ya usalama barabarani Peter Sima aliwataka madereva hao kutoa taarifa haraka polisi ikiwa dereva amemtilia shaka abiria liye mpaki katika pikipiki yake ili kuweza kutia mbaro watekaji wa
pikipiki na wauwaji wa madereva hao.
Aidha aliwataka madereva hao kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria za
barabarani ikiwa ni pamoja na kuwa na leseni zinazo waruhusu kufanya
biashara hiyo na leseni ya kuendesha chombo hicho jambo ambalo litapunguza
ajali za mara kwa mara.
pikipiki na wauwaji wa madereva hao.
Aidha aliwataka madereva hao kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria za
barabarani ikiwa ni pamoja na kuwa na leseni zinazo waruhusu kufanya
biashara hiyo na leseni ya kuendesha chombo hicho jambo ambalo litapunguza
ajali za mara kwa mara.