Festus Pangani, Njombe
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilayani Njombe jana
imewafikisha mahakamani viongozi watatu wa Mtaa wa Wikichi Kata ya
Ramadhani Akiwemo Afisa Mtendaji wa Kijiji Hicho Bw Zabron Mgeyekwa
Akisoma
Hati ya Mashtaka Mahakamani Hapo, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU
Wilayani Njombe Richard Marekani Amewataja Watuhumiwa Wengine Kwenye
Kesi Hiyo Kuwa ni Pamoja na Willy Ngaro Aliekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Shule ya Msingi Wikichi na Emmanuel Mwalongo Aliekuwa Mwenyekiti wa
Kijiji cha Wikichi
Akifafanua
Zaidi Mahakamani Hapo Mwendesha Mashtaka Huyo Ameiambia Mahakama Kuwa
Mnamo Mwaka 2007 Kwa Pamoja Wakiwa ni viongozi wa kijiji waliwatoza
wananchi wa kijiji hicho Michango ya Zaidi ya shilingi laki mbili Huku
stakabadhi ya malipo Ikionesha Kuwa Michango Iliyochangwa ni Shilingi
Elfu 38 Tu.
Kesi
Hiyo iliahirishwa Hadi Agost 23 Baada ya Watuhumiwa Kukana kuhusika na
Makosa Hayo na Hivyo Kurudishaw Mahabusu Baaada ya Kukosa Wadhamini.
Akizungumza
Nje ya Mahakama Hiyo Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Wilaya ya Njombe
Richard Marekani Amesema Watuhumiwa hao Kwa Pamoja Wanatuhumiwa Kwenda
Kinyume na Sheria ya Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007.
Katika
Hatua Nyingine Taasisi ya Kuzuia n Kupambana na Rushwa TAKUKURU
Wilayani Njombe imewataka Wananchi Kuendelea Kushirikiana na Taasisi
Hiyo Katika KUwafichua na KUwataja Watu Wanojihusisha na vitendo Vya
Rushwa Kama Njia ya Kusaidia Kupunguiza Tatizo la Rushwa Mkoani Hapa