Watumishi nane wa jiji la Mbeya watimuliwa kazi.

Kenneth Ngelesi na Angelika Sullusi, Mbeya

HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, kupitia Baraza la Madiwani limewafukuza kazi  watendaji nane,na kuwapo omnyo kali ilkiwa na kushuhwa dara kwa baadhi ya watumishi  wakiwemo watumishi watatu wa  Idara ya Uhasibu kwa tuhuma za kujipatia fedha isiyo halali kiasi cha zaidi ya shilingi mil 35 ikiwa mishara hewa.
Hatua ya kuwa timu kazi kazi watushi hai ilifikiwa jana na baraza hilo ktika kamati kuu kuu ya Baraza hilo Ambapo watumishi hao wanatuhumiwa kuiba fedha ambazo fedha za mishahara ya watumishi ambao hawakustahili kulipwa fedha hizo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kustaafu, kuacha au kuachishwa kazi pamoja na kufariki na hivyo fedha hizo zilitakiwa kurejeshwa hazina.
Katika kashfa hiyo inawajhusisha Sarah Kibona Mhasibu mwandamizi,Tito Robart Mwakisole Mhasibu daraja la kwanza pamoja na  Petro Ulamso Yohana ambaye ni mlinzi amabaye akaunt yake ilituymika kupitishia fedha hizo katoka bank ya NMB tawi la Mbalizi Roads .
Tamko la kufukwa kazi kwa watendaji hao lilitolewa na, Meya wa Jiji la Mbeya Athanasi Kapunga, kwenye kikao cha Baraza la Madiwani mara baada ya kukaa kama Kamati ya  kuwajadili watumishi hao ambapo Meya huyo alisema baraza limepekeza kufukzwa kazi na wengini kupoewa onyo.
Alisema, Sara Kibona pamoja na Tito Robert wanakabiliwa na shitaka (kanuni 42) kujipatia fedha isiyo halali (wizi)kiasi cha sh. 35,328,314. na shitaka la pili kwa mujibu wa (kanuni ya 42) kushindwa kutimiza wajibu au kutekeleza maelekezo aliyopewa na mwajiri wake wa kazi na hivyo kusababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha.
Alisema, watuhumiwa wote wanadaiwa kutumia fursa ya cheo chao kwa kushirikiana na mtumishi wa Benki ya NMB kuiba fedha za mishahara ya watumishi wasiostahili kulipwa kwa kuingiza mishahara hiyo kwenye akaunti za watu mbalimbali pamoja na za kwao wenyewe.
Aidha, Meya huyo alisema kuhusu mlinzi Petro Ulamso yeye akaunti yake inadaiwa kutumiwa na wahasibu hao kwa kuingiziwa fedha shilingi milioni 3,875,350 ambazo ni mali ya mwajiri.
Alisema, pia mlinzi huyo anakabiliwa na shitaka la pili la kushindwa kutimiza wajibu akiwa kama mlinzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya na kushindwa kutoa taarifa ya kuingizwa kwa kiasi hicho cha fedha isivyo halali kwa mwajiri ili zirejeshwe serikalini.      
Mbali na watushi hao afisa mwingile aliye fukuzwa kazi ni Joseph Ndaki kwa tuhuma za kughushi taarifa za uthamini wa ardhi kwa ajili Tasisisi ya Sayansi na Teknologigia (MIST) katika eneo la Ikuti na Inyala na  kuidanganya serikali kwa kusudio la kujipatia  fedha bil 5,111,164,373  kwa manufaa yake.
Alisema, Ndaki alikuza eneo la uthamini pasipo uhalali na kwamba hekta 72 ndizo alipaswa kuzifanyia kazi lakini yeye aliingiza hekta 190 kwa maslahi yake mwenyewe na hivyo baraza limependekeza afukuzwe kazi.
Hata hivyo,  katika hatua nyingine Baraza hilo limependekeza kufukuzwa kazi kwa Afisa mtendaji wa kata ya Ilemi kwa wizi wa shilingi milioni 1.5. pamoja na afisa mtendaji wa Mtaa ya Ilindi kwa kuhusika na wizi wa milioni 1.5 kwa kudaiwa kutumia bila ridhaa  ya kamati fedha za miradi ya maendeleo.
Aidha katika hatua nyingine baraza hilo limemshusha daraja afisa mten adji wa kata ya Iziwa kwa tuhumna za mwenendo mzuri akatika kazi ikiwa ni pamoja na ulevi na utoro kazini na kumta onyo afisa mtenadaji kata Mbalizi Road


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo