WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO MAKETE WAPEWA SOMO

MAKETE

Wamiliki wa vyombo vya moto wilayani Makete wametakiwa kufuata taratibu zote za umiliki wa vyombo hivyo ili kuondokana na usumbufu usio wa maana pamoja na kuepuka ajali zisizo za lazima

Hayo yamesemwa na Meneja wa mamlaka ya mapato TRA wilaya ya Makete Halid Kimolo katika kiako cha wamiliki wa vyombo vya moto kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete kikiwa na lengo la elimu ya umiliki wa vyombo hivyo na utoaji wa leseni

Bw. Kimolo amesema wamiliki wote wanatakiwa kuzingatia vitu vya muhimu kama vile leseni ya chombo chake, kadi pamoja na uendeshaji salama kuongeza kuwa leseni inatakiwa kuwa na majina matatu ya mmiliki wa chombo hicho

Amesema kama kuna mtu anatilia shaka uhalali wa nyaraka za chombo cha usafiri anatakiwa kufika mamlaka ya mapato wilayani hapo kujiridhisha zaidi ili kupata uhakika

Amewataka wamiliki wa vyombo hivyo kutobadilisha majina yao kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha usumbufu katika utendaji kazi

Na Kumbuka Kilando & Raphael Abel


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo