Na Global Publishers
WAKIMBIZI kutoka Somalia zaidi ya 100
waliokuwa wakisafiri kwa kificho kutoka Ethiopia kwenda nchi za Malawi
na Afrika Kusini kwa lengo la kusaka maisha bora baadhi yao walipoteza
maisha hivi majuzi baada ya kukosa hewa wakati wakisafirishwa kwenye
kontena ili kuwakwepa maofisa wa Idara ya Uhamiaji nchini.
Tukio hilo lilitokea katikati ya wiki hii mkoani Dodoma ambapo Wasomali 44 waligundulika kuwa wamekufa na 72 wakiwa wamenusurika.
Miili hiyo iliyokuwa imeanza kutoa harufu, 22 ilizikwa Dodoma na 22 ilizikwa Ijumaa wiki hii mjini Morogoro katika makaburi ya Kolla ilikopewa mazishi ya jumla ya Kikristo na Kiislam.

PICHA/HABARI:
DUNSTAN SHEKIDELE, GPL, MOROGORO