MAHAKAMA ya wilaya ya Lindi,imempatia
dhamana mshitakiwa Aluminata Alois Kimisa (38) anayekabiliwa na Shitaka
la kujaribu kumuuwa mtoto wake mchanga aliyemzaa usiku wa mei 19 mwaka
huu.
Mwandishi kutoka Lindi Abdulaziz Video
anaripoti kuwa ,Uamuzi wa kumpatia dhamana mshitakiwa huyo umetolewa
mei 28 mwaka huu na Hakimu wa mahakama ya wilaya hiyo,Liliani
Lugalabamo, baada ya kupitia vifungu mbalimbali vya Sheria.
Mshitakiwa
Aluminata mei 22 mwaka huu,alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na
Shitaka la kujaribu kumuuwa mtoto wake kwa kumtumbukiza kwenye Shimo la
Choo.
Akitoa
uwamuzi huo,Hakimu Lugabamo akitumia ibara ya 6 na 7 ya Human right
alisema kila mtu ana haki sawa mbele ya Sheria,hivyo kutokana na
mshitakiwa ana mtoto mchanga ambaye anatakiwa kuwa karibu zaidi na mama
anampatia dhamana,huku akiamuru kupatiwa mtoto wake kwa ajili ya
kumnyonyesha.
Pia Hakimu huyo amemuagiza mshitakiwa huyo kuripoti mahakamani hapo kila siku ya ijumaa saa 2:30 asubuhi.
Mwanamke
huyo amefikishwa katika mahakama ya mkoa huo,mei 22 mwaka huu,na
kusomewa shitaka lake na mwanasheria wa Serikali, Juma Maige.
Aluminata
alitinga mahakamani hapo, akiwa amevalia nguo aina ya vitenge na
kujifunika kanga huku kichwani akiwa amefunika nywele zake kwa mzura wa
rangi ya kahawia,huku dada zake wakiwa wamekibeba kichanga hicho.
Na www.francisgodwin.blogspot.com