Mamalioni wa shilingi yatafunwa na watenadaji wa kijiji Ntokela, Rungwe

WIMBI la kuondolewa kwa vingozi wa serikali za vijiji limeendelea kushika kasi katika wilaya ya Rungwe baada ya wanakijiji cha Ntokela katika kata Isongole wilaya hapa kugoma kujishughulisha na shughulki zote na maendeeo mpaka uongozi wa kijiji hicho utakapo anjia nafasi zao za uongozi.

Wananchi  hao wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini ubadhilifu wa fedha takribani mil  60 ambazo ni mali ya kijiji hicho ambazo zimetokana wa mapato ya miradi mbalimbali ikiwemo ushuru wa mashamba ya kijiji kwa mwaka 2010 hadi 2012.

Wamesema kuywa fedha hizo zimetafunwa na mwenyekiti wa kiji hicho kwa kushirikiana na wajumbe wa serikari ya kijiji,vitongo wapatao nane kutoka kijiji hicho kwa kushikian afisa matendaji wa kata hiyo walie mpyta kwa jina la Charlesi Mwamaso ambaye amesimamishwa kazi na baraza klla madiwani wa wilaya hiyo katika kikao cha bajewi mwishoni mwa mwezi April
.
Wanacnhi hao wameda kuwa  walishtukia wizi huo wa mamilioni ya fedha baada ya  machi 4 mwaka huu kuulazimisha uongozi wa kijiji hicho kusoma  mapato na matumizi  baada ya kutofanya hivyo kwamudamrefu na kubaini kiasi hicho cha shilingi milioni 64.5 kilikuwa kidogo ukilinganisha na vyanzo vilivyopo.

Mmoja wawananchi hao Christone Tweve ,alisema baada ya kuishtukia taarifa hiyo ya
mapato na matumizi walilazimika kuunda tume ya watu 12 ambayo baada ya kufanya uchunguzi ilibaini wizi huo hali iliyochochea wananchi kuamua kususia shughuli za maendeleo.

“Tulimaua kuunda tume hiyo kwa lengo la kujiridhisha na matumiza ya yalifanywa na vingozi hao na hiyo ilifanyika mwezio wa kwanza na ripoti ya tume hiyo ambayo tulicxhanganya waju,mbe kutoka serkari ya kijiji na na rai wa kawaida na ripoti hiyo iliwaslishwa mwezi machi 4 mwaka huu na kubaini madudu hayo ndipo wananchi wakaamua kususia shulizote za maendelkeoa wala kutoa michango, hata kulipa ushuru
 pamoja na michango mbalimbali kwa ajili ya maendeleo wakishinikiza uongozi mzima wa kijiji kuachia ngazi’  alisema Tweve

Hata hivyo waandishi wa habari walimua kitafuta  mmoja wa wajumbe wa tume hiyo, aliyejitambulisha kwa jina la Rudwel Mtweve, ambaye alikiri kuhusika na uchunguzi wa tuhuma hizo za wizi
akiwa kama mjumbe.

Alisema katika mradi wa kukodisha shamba la kijiji lenye ukubwa wa Hekari 57 jumla ya
shilingi milioni tatu zimebainika kutafunwa katika msimu wa kilimo wa mwaka 2011 hadi 2012.
“Unajua katika wilaya yetu ya Rungwe Mungu ametubariki tunalima mara mbili kwa msimu, ambapo kuanzia Machi hadi Julai huwa tunalima viazi na  Augost hadi Februari huwa ni zamu ya kulima mahindi hivyo kipindi chote shamba hili la kijiji huingiza fedha kutoka kwa
wakodishaji”.

Mtweve alifafanua kuwa katika miezi ya kulima viazi wakulima hukodi shamba hilo kwa
kiasi cha shilingi 150,000 kwa Ekari  moja na miezi ya kulima mahindi pia kila Ekari hukodishwa kwa shilingi 80,000 katika shamba hilo lenye ukubwa wa Ekari 57.
Alitajambinu nyingine iliyotumiwa na uongozi huo wa kijiji kuiba fedha hizo ni kuwa na vitabu vya aina mbili vya kukusanyia ushuru, ambapo kitabu kimoja ni cha halimashauri na kingine kinaonekana kununuliwa kutoka mtaani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Meckson Mwakipunda, alipoulizwa juu ya
sakata hilo kwa njia ya simu yake ya mkononi alikiri  kwa uongozi huo kutafuna fedha za ushuru kiasi cha shilingi milioni saba.
Alisema baada ya hali hiyo halmashauri imeanza kuchukua hatua , ikiwemo kumsimamisha kazi  Mwenyekiti huyo Kijiji baada ya wakaguzi wa ndani kubaini wizi huo, ampapo alidai mbali na Mwenyekiti huyo pia kuna baadhi ya viongozi wa kata nao wanaonekana kuhusika na ndiyo maana afisa mtendaji  ni moja ya watumishi waliosimamishwa kazi na baraza adiwani wakati wa kikao cha baget mwezi kwa ubadhilifu wa fedha za uma.

“Ni kweli ndugu wandishi wa habari hayo unayoniuliza nayafahamu kwa kina na hatua ndio
hizo tumechukua, lakini kama kumehibuka hilo la kususia shughuli za maendeleonitamtuma Mkurugenzi wangu afike kijijini hapo ili kufikia muafaka”  alisema Mwakipunda.

Hatua hiyo ya wana kijijio cha Ntokela imekuja ikiwa ni juma moja limepita tangu wanachi wa kijiji Ilundo kata ya Kiwila wolyani hapa kuzoba njia kwa kuweka magogo barabarani kwea kunikisha kuondolewa katika nafasi  ya uwenyiki  mwenyekiti wa kijiji hichoi alifahamika kwa jina la Mwangosi na P[olisi kulazimika kutmia mabomu kuwa tawaya wananchi hao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo