MWALIMU AFUMWA AKITAKA KUMBAKA MWANAFUNZI

Makete

Mwalimu wa shule ya sekondari Iwawa wilayani Makete aliyefahamika kwa jina la Deodatus Mvile anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani hapa kwa tuhuma za shambulio la aibu kwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 anayesoma kidato cha pili shuleni hapo

Akizungumza na mtandao huu mkuu wa polisi wilaya ya Makete Bw, Peter Kaiza amesema tukio hilo lilitokea Ijumaa usiku Juni 15 mwaka huu katika ofisi ya mwalimu huyo 

Amesema kuwa mwalimu huyo alikuwa katika hatua za mwanzo za kutaka kufanya ngono na mwanafunzi huyo hivyo kushikwa na wanafunzi waliokuwa shuleni hapo ingawa alikuwa bado hajafanya kitendo hicho

"Ni kweli tunamshikilia mwalimu huyo na katika mahojiano na uchunguzi wetu wa awali umeonesha kuwa, bado alikuwa hajafanya kitendo hicho ndio maana tumemfungulia mashitaka ya shambulio la aibu dhidi ya mwanafunzi wake" alisema Kaiza

Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na mtuhumiwa yupo nje kwa dhamana na atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka muda wowote kuanzia sasa
Hii ni mara ya pili kwa mwalimu huyo kuhusishwa na matukio kama hayo kwa matra ya kwanza mwalimu huyo alikutwa chumbani kwa mwanafunzi mwingine akitaka kufanya naye ngono, lakini haikufahamika tukio hilo liliishia wapi hadi alipofumaniwa tena kwa mara ya pili

 Na: Veronica, Teddy & Ester


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo