Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Doktafu
Mbilinyi mkazi wa Ikonda wilayani Makete anashikiliwa na polisi wilayani Makete kwa tuhuma za kumchoma moto
mtoto wake wa kumzaa
Kwa mujibu wa mkuu wa polisi wilaya ya Makete Bw,
Peter Kaiza amesema tukio hilo
lilitokea siku Juni 5 mwaka huu ambapo mama huyo alikamatwa katika hospitali ya Consolata Ikonda
alikompeleka mtoto huyo kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kuona ameshindwa kumtibu
kwa njia za kienyeji
Kwa mujibu wa maelezo ya mama huyo amesema mtoto
wake aliungua moto wakati akicheza na mtoto mwenzie na si kama amemuunguza yeye
Mama huyo yupo nje kwa dhamana na muda wowote atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili
Na Veronica Mtauka, Teddy & Ester
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube