Makete
Wananchi wilayani Makete wametakiwa kujikinga na
maambukizi mapya ya vvu kwa kuacha tabia hatarishi zinazopelekea mtu kupata
ugonjwa wa UKIMWI
Hayo yamezungumzwa na mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya ya Makete Mh, Daniel Okoka wakati akizindua kituo cha CTC katika
zahanati ya kata ya Mfumbi nakusema lengo la kujengwa kwa kituo hicho ni kuweka
huduma karibu na watu walio na maabukizi ya vvu
Katika uzinduzi huo pia Mh Okoka alikabidhi
pikipiki aina ya bajaji katika zahanati hiyo ili iweze kubeba wagonjwa
waliozidiwa na kuwapeleka katika hospitali kubwa kwa haraka hasa wanawake ili
kupunguza vifo vya kina mama na watoto na kuwataka waitunze pikipiki hiyo
Naye diwani wa kata ya Mfumbi Mh. Athilio Ng'ondya ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete akiongea
kwa niaba ya wananchi ameishukuru serikali kupitia idara ya afya Makete
kwa kuamua kuwapa pikipiki na kuahidi kuwa wataitunza na kuitumia vizuri
kwa kila mtu bila kujali kipato cha mtu wala cheo
Na: Obeth
Ngajilo