Askofu Levis Sanga akipewa uaskofu
Askofu Levis (mwenye fimbo) akiwa na maaskofu wenzie
Askofu Sanga akipongezwa na mkewe
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapt. Mstaafu Aseri Msangi akimpa mkono baba askofu
Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akimpa mkono baba askofu
Hapa msaidizi wa askofu akipewa usaidizi wa askofu
Askofu Levis Sanga (kushoto) akiwa na Msaidizi wa Askofu Mch. Kahuka
Askofu Sanga akitoa hotuba yake
RC NJOMBE
DC MAKETE
Askofu wa Dayosisi ya kusini Kati
Mch. Levis Luhuvilo Sanga hii leo amesimikwa rasmi kuwa Askofu na mkuu wa
Dayosisi hiyo pamoja na Mch. Philemon Kahuka kuwa msaidizi wa askofu wa
dayosisi ya kusini kati
Tendo hilo limefanyika katika viwanja vya kanisa
kuu Makete mjini na kuhudhuriwa na Mkuu wa kanisa la KKKT Dkt. Alex Malasusa,
Mkuu wa mkoa wa Njombe ambaye pia alimwakilisha mgeni rasmi Mizengo Pinda,
maaskofu mbalimbali na wasaidizi wao, mkuu wa wilaya ya Makete, viongozi
mbalimbali wa dini pamoja na waumini wa madhehebu mbalimbali
Askofu aliyemaliza muda wake Dkt.
Hans Mwakabana ndiye aliyeongoza tendo la kumsimika kazini Askofu Levis Sanga
Pia Mkuu wa Kanisa La kiinjili la
kilutheri Tanzania Dkt. Alex Malasusa alimsimika askofu Levis Sanga kuwa mkuu
wa Dayosisi ya kusini Kati
Baada ya tendo hilo
Askofu Levis
Sanga alimsimika kazini msaidizi wa askofu Mch. Philemon Kahuka
Kukamilika kwa tendo hilo la kuwasimika kazini
viongozi hao zilifuata salamu mbalimbali ikiwemo hotuba ya askofu Levis Sanga
pamoja na hotuba ya Mgeni rasmi waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Mh. Mizengo Pinda iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapten Mstaafu Aseri
Msangi
Akitoa hotuba yake kwa mamia
waliofurika katika viwanja vya kanisa kuu Makete mjini Askofu Sanga amesema
kanisa litaendelea kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto
mbalimbali zikiwemo za afya na elimu kwani kwa sasa kanisa kupitia dayosisi ya
kusini kati linaanzisha chuo cha ualimu Bulongwa kitakachotoa mafunzo ya ualimu
kwa ngazi ya stashahada na cheti daraja la tatu A na chuo hicho muda wowote
kuanzia sasa kitaanza kutoa mafunzo hayo
Pamoja na mambo mengine amesema
kuwa kanisa linaendelea kutoa elimu ya namna wananchi watakavyotoa maoni yao katika mchakato wa
kuanzisha katiba mpya kwani ni wajibu pia wa kanisa kufanya hivyo
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa
Njombe Kapten Mstaafu Aseri Msangi ambaye alimuwakilisha mgeni rasmi waziri
mkuu Mizengo Pinda alianza kwa kumtambulisha mkuu mpya wa wilaya ya Makete Mh.
Josephine Matiro pamoja na kuwahakikishia wananchi kuwa serikali inatambua
mchango wa kanisa katika kusukuma gurudumu la maendeleo hapa nchini
Amesema kuwa anakaribisha maoni ya wananchi kufanikisha
maendeleo ya mkoa wa Njombe pamoja na kuhakikisha kuwa atasimamia urasimu
uliopo katika kuanzisha taasisi mbalimbali hasa za kidini ikiwemo vyuo na shule
ama hospitali
Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi
kujitokeza kwa wingi katika kufanikisha sensa ya watu na makazi na kuwataka
wananchi wote kushiriki ipasavyo
Akitoa shukrani kwa Mgeni rasmi
Mkuu wa KKKT Dkt. Alex Malasusa amefurahishwa na ushirikiano uliooneshwa na
Mkuu wa mkoa wa kushirikiana na kanisa na kuongeza kuwa lengo la kanisa ni
kuhakikisha viongozi wote wanamjua Mungu ili wafanye kazi zao kwa uweza wa
Mungu